Idara ya utumishi na Utawala inatekeleza kazi mbalimbali zikiwemo uandaaji wa bajeti ya Mishahara ya watumishi na kuziwasilishwa Ofisi ya Rais UTUMISHI,TAMISEMI na HAZINA kwa ajili ya kupitishwa.Pia imekua ikifanya kazi mbalimbali za mfumo ikiwa ni pamoja na kusafisha taarifa za Watumishi na kuwaondoa Watumishi waliostaafu,kufariki na kupata uhamisho.