Idara ya kilimo,Umwagiliaji na Ushirika ni miongoni mwa Idara zinazotoa huduma katika jamii.Idara inatoa ushauri wa mafunzo kuhusu kilimo bora,Kilimo cha Umwagiliaji na Ushirika kwa lengo la kuiwezesha jamii kupata tija katika za uzalishaji wa mazao ili kuhakikisha kila kaya inajitosheleza kwa chakula,inaongeza kipato hivyo kupunguza umaskini katika jamii.
Aidha hutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundo mbinu ya Umwagiliaji,Masoko,Maghala na kusimamia Miradi ya Vikundi vya Uzalishaji wa mazao ya chakula na Biashara na Ujasiriamali.
Katika kipindi cha mwezi januari hadi machi 2017 idara ilitekeleza majukumu yake kwa kutumia fedha kutoka kwa wahisani ili kuendeleza zao la korosho,swisscontact na MIVARF.
Hali ya chakula kwa sasa ni ya wastani,Wananchi wanapata chakula kila siku upungufu wa chakula umejitokeza katika baadhi ya maeneo kutokana na kuchelewa kunyesha mvua za vuli kuliko sababishamazao ya Mahindi na Mapunga wa mlimani kuchelewa kukomaa mpaka sasa.Vile vile mavuno katika msimu wa kilimo 2015/2016 kutofikia lengo kutokana naupungufu wa mvua za vuli na masika,Ingawa wanaendelea kushauriwa kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda mazao yanayokomaa kwa muda mfupi,kupanda mazao ya kinga ya njaa kama Mihogo,Viazi Vitamu,Ndizi,Magimbi na Mahindi ya muda mfupi.Wakulima wakifuata ushauri huu upungufu wa unaweza kupungua kwa kiasi kikubwa.
SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NI KAMA IFUATAVYO:
Kuhamasisha Wakulima kuupokea na kuutekeleza mpango wa upandaji mikorosho mipya kwa muda wa miaka 3 kuanzia msimu 2016/2017 hadi 2018/2019 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri mkuu Mh.Majaliwa Kassimu Majaliwa kwa bodi ya korosho na Mfuko wa WAKFU.
Usambazaji na Umwagiliaji wa miche ya korosho imenufaisha zaidi ya wakulima 1,606 hadi sasa tarafa za Vigoi,Mwaya,Ruaha na Lupiro kama ifuatavyo:
Ugawaji wa miche bado linaendelea kwa baadi ya vijiji
KITENGO CHA USHIRIKA:
Wilaya ya Ulanga ina jumla ya vyama vya Ushirika 66 vilivyosajiliwa kwa mujibu wa sheria ya Ushirika Na.6 ya mwaka 2013.kati ya hivyo 27 ni sinzia.
AMCOS 10 {Hai 6,sinzi/kufa 4}
SACCOS 39{Hai 21,sinzia/kufa 18}
Vyama aina nyingine 15{Hai 10,sinzia/kufa 5}
IDARA IMETATUA CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA KAMA IFUATAVYO:
{a} Kuendelea kuzishawihi Taasisi zisizo za kiserikali kama MIVARF,Swisscontact na VISTA kushiriki katika kutatua matatizo ya Wakulima na kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo.
{b} Kuendelea kuwaelimisha Wakulima kupanda mazao yanayostahili ukame na yanayokomaa kwa muda mfupi.
{c} idara itaendelea kushirikiana na Serikali kuu kusimamia upatikanaji pembejeo na kuchagua mawakala wenye uwezo wa kusambaza pembejeo hizo kwa Wakulima kwa wakati.
{d} mkandarasi ameshauriwa kusimamia kazi ili kusubiri kina cha maji kipungue.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.