1.6 Muundo wa Utawala:
Halmashauri ya Ulanga ina Tarafa nne (4) yenye Kata = 21,Hospitali 1,Shule za Sekondari = 21,Zahanati 21,Shule za Msingi = 59 ,Vijiji = 59, Idadi ya Watu = 151,001 ,Vituo vya Afya = 2.
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Ulanga ambalo ni chombo cha juu cha kutolea maamuzi lina jumla ya Madiwani 21. Kati yao Madiwani 16 ni wa kuchaguliwa kutoka kata 21 za Halmashauri.
Katika mfumo wa Utendaji, Manispaa ya Morogoro ina Idara kumi na tatu na Vitengo sita vinavyowajibika moja kwa moja kwa Mkurugenzi. Idara kumi na tatu za Halmashauri ni:
1) Utawala na Utumishi
2)Fedha na Uongozi
3)Afya
4)Elimu Msingi
5) Elimu Sekondari
6) Mipangomiji na Ardhi
7) Maji
8) Maendeleo na Ustawi wa Jamii
9) Mifugo na Uvuvi
10)Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
11)Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
12)Usafi na Mazingira
13)Ujenzi na Zimamoto
Vitengo vitano ni:-
1) Sheria
2) Ukaguzi wa Ndani
3) Ugavi
4) Uchaguzi
5) Ufugaji Nyuki
6) Teknologia,Habari, Mawasiliano na Uhusiano
Ulanga kama chombo cha utawala, kinatawala kwa mtindo wa Kamati. Kuna Kamati kuu tano ambazo ni
i) Kamati ya Fedha na Uongozi
ii) Kamati ya Huduma za Uchumi, Elimu na Afya
iii) Kamati ya Mipangomiji na Mazingira
iv) Kamati ya kudhibiti Ukimwi
v) Kamati ya Maadili.
1.7 Idadi ya Watumishi:
Kwa Mwaka 2010/2011, Halmashauri ina jumla ya watumishi 3123 wa kada mbalimbali.Idara ya Elimu (Msingi na Sekondari) ina watumishi 2425 sawa na asilimia 77.6 ya watumishi wote.
2.0 Maendeleo ya Kisekta
Sekta zote za Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro zinatekeleza majukumu yake ya msingi kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2011 - 2015, Dira ya Maendeleo ya 2025, Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) II na Malengo ya Millenia ili kutoa huduma bora kwa jamii. Maelezo ya kila sekta yameainishwa kama ifuatavyo.
RAMANI IKIONYESHA ENEO LA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.