MAWANDA YA KAZI ZA UKAGUZI WA NDANI
Mawanda ya kazi za ukaguzi wa ndani yameainishwa katika kanuni namba 34 ya kanuni za Fedha za umma ya mwaka 2004,Agizo namba 4 la Memoranda ya Fedha ya serikali za mitaa ya mwaka 2009 na Muongozo wa ukaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2013.
v Mkaguzi wa Ndani ataandaa mpango wa mwaka wa ukaguzi wa Ndani na nakala itapelekwa kwa Mkaguzi na Mdhitibiti wa Hesabu za Serikali, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali na Katibu tawala wa Mkoa siyo zaidi ya tarehe 15 ya Julai ya kila mwaka.
v Mkaguzi wa Ndani ataandaa mpango wa mwaka wa ukaguzi wa ndani unaonyesha vihatarishi na kuuwasilisha kwa Kamati ya Ukaguzi na Afisa Masuhuri kwa uthibitisho.
v Mkaguzi wa ndani atapitia na kutathmini mpango wa bajeti na utekelezaji wake ili kupima kama inakidhi shabaha na Malengo ya Taifa na Halmashauri,taarifa za kitaalamu katika shughuli za maendeleo,kazi,bidhaa na huduma zitolewazo kwa halmashauri katika maendeleo na utekelezaji wa bajeti kwa kuzingatia thamani ya Fedha.
v Mkaguzi wa Ndani hata fanya ukaguzi au uchunguzi bila ya kuandika mpango wa ukaguzi unaoonyesha yafuatayo;
a) Kichwa cha habari cha mpango wa ukaguzi.
b) Malengo ya ukaguzi
c) Taratibu zitakazotumika katika kukagua kwa mtiririko.
v Kupitia uhalali na usahihi wa taarifa za Fedha na utendaji wake,na namna taarifa hizo zilivyopatikana;
a) Kupitia na kutoa taarifa juu ya udhibiti wa makusanyo utunzaji na matumizi ya rasilimali fedha za Halmashauri.
b) Kupitia na kutoa taarifa juu ya kufuatwa kwa taratibu za fedha zilizowekwa, sheria maagizo na taratibu za kihasibu zinazotolewa na Waziri katika nyakati mbalimbali ili kuwepo kwa matumizi mazuri ya fedha.
c) Kupitia na kutoa taarifa juu ya usahihi wa mpangilio na mgawanyo wa mapato na matumizi ya akaunti.
d) Kupitia na kutoa taarifa juu ya usahihi na uaminifu wa takwimu za fedha zilizotumika katika kuandaa taarifa za fedha na taarifa nyingine.
e) Kupitia na kutoa taarifa juu ya mifumo iliyopo inayotumika kutunza mali.
v Mkaguzi wa ndani anapaswa kuhakiki na kutathmini taarifa za mwisho za Fedha ,kupima mfumo wa udhibiti wa Fedha ufanisi wake katika Fedha za umma kama ilivyoainishwa katika muongozo wa taaluma wa kimataifa(IPPF) ,fungu namba 2130 la ukaguzi wa ndani kwa kupitia yafuatayo:
a) Mfumo wa udhibiti wa ndani.
b) Uwasilishwaji wa taarifa zote za Fedha
c) Utoaji wa taarifa za Fedha unakidhi misingi ya uhasibu
d) Uthibitisho wa rasimali na madeni ya halmashauri unaambatana na ushaidi wa nyaraka.
e) Rasilimali,madeni,mapato na matumizi yanawasishwa kwa ushihi kwenye taarifa za Fedha
f) Rasilimali na madeni yaliyoripotiwa yanamilikiwa na halmashauri
g) Ukamilifu wa taarifa za Fedha za halmashauri wa kipindi husika
h) Usahihi wa upimaji na tathmini ya taarifa za rasilimali,madeni,mapato na matumizi
i) Uhakiki wa nyaraka za Fedha.
v Mkaguzi wa Ndani atatunza rejista ya kazi alizofanya ikionyesha tarehe ya kufanya kazi za nje, tarehe ya kutoa tarifa ya mwisho na aina ya majibu yaliyopokelewa kwa hoja mbalimbali na kuonyesha ufuatiliaji wake.
v Mkaguzi wa Ndani ataandaa na kuwasilisha taarifa ikionyesha tarehe moja kwa moja kwa Afisa masuhuri kwa utekelezaji wake na kuiwasilisha katika Kamati ya Fedha.Afisa masuhuri atapeleka nakala kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Serikali, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali na Katibu Tawala wa Mkoa ndani ya siku 15 za kazi toka tarehe ya kupokea taarifa.
v Mkaguzi wa Ndani ataandaa na kuwasilisha taarifa mbili za ukaguzi kwa Afisa masuhuri;
a) Taarifa ya robo itawasilishwa kwa Afisa masuhuri ndani ya siku 15 baada ya robo kwisha na.
b) Taarifa ya mwaka itawasilishwa kwa Afisa masuhuri ndani ya siku 15 baada ya mwaka kwisha.
v Baada ya taarifa ya ukaguzi kuaandaliwa na kusainiwa na Mkaguzi wa Ndani, itawasilishwa kwa Afisa masuhuri, nakala ya taarifa hiyo itawasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Serikali, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali,Katibu Mkuu TAMISEMI,na Katibu tawala wa Mkoa kwa barua.
v Mkaguzi wa Ndani hatampa au kutoa taarifa kwa mtu ambaye hastahili kuwa na taarifa hizo.
v Mkaguzi wa Ndani atafanya kazi zake kitaaluma na maoni na ushauri vitataolewa baaba ya kufanya utafiti ya kutosha na yatakwenda kwa afisa anayehusika na sehemu husika.bila kufuata taaluma na maadili Mkaguzi wa Ndani atahusika kwa lolote litakalo sababishwa na taarifa yake.
v Mkaguzi wa Ndani atahudhuria vikao vya menejimenti vinavyfanyika katika Halmashauri.
HAULE.L.J
MKAGUZI MKUU WA NDANI
HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.