Idara ya Maendeleo ya Jamii ni Idara mtambuka ambayo imelenga katika kuiwezesha jamii kubaini uwezo wao,matumizi yao na kutumia rasilimali zilizo kwenye maeneo yaoili kujiletea maendeleo.Katika kufanikisha lengo hili,Idara hutumia mbinu za uraghibishi,uwezeshaji,uhamasishaji,utetezi na ushirikishwaji jamii katika mchakato wa kutekeleza shughuli za kuwaletea watu maendeleo endelevu.
SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA;
Kuratibu na kusimamia mfuko wa Wanawake kwa njia ya kutoa elimu ya ujasiriamali,mikopo na kufuatilia marejesho kwa vikundi vya wanawake wajasiriamali vilivyokopeshwa kutoka mfuko wa maeneleo ya wanawake{WDF}kwa mwaka 2015/2016 na 2016/2017.
KITENGO CHA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI;
Kitengo cha mashirika yasiyo ya kiserikali kina jukumu la kuratibu shughuli zote zinazotekelezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali katika Wilaya ya Ulanga.Aidha kitengo hiki husajili vikundi vyote vya uzalishaji mali kwa lengo la kuvitambua na kuchangia pato la ndani la Halmashauri.ili kikundi kiweze kusajiliwa na kupatiwa cheti cha usajili hutakiwa kuwasilisha vielelezo muhimu kama vile;barua ya maombi ya usajili,utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti/Mtendaji wa Kijiji/Kata,muhtasari wenye azimio la kusajili kikundi,katiba iliyopitiwa,kusainiwa na kugongwa muhuri na Hakimu/Mwanasheria,picha za viongozi;gharama za usajili ambayo ni Tsh.40,000/=.
KITENGO CHA UKIMWI;
Kitengo kina jukumu la mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kuratibu shughuli za mapambano dhidi ya UKIMWI katika sekta mbalimbali ndani ya Wilaya ili kuweza kutokomeza janga hili.Pia kitengo kimekua kikitoa elimu ya kujikinga na UKIMWI kwa makundi mbalimbali na jamii kwa ujumla,kutoa huduma mbalimbali za kupunguza makali yatokanayo na UKIMWI kwa kutoa misaada kwa WAVIU na watoto waishio katika Mazingira hatarishi{WWKMH}pamoja na ugawaji wa kondom.
Pia imetoa elimu ya kujikinga na Virusi vya UKIMWI na magonjwa ya ngono kwa makundi yaliyo katika hatari hatari ya kupata maambukizi ya VVU ambao ni wahudumu wa mabaa na nyumba za kulala wageni kwa tarafa ya Malinyi,Vigoi,Mtimbira na Lupiro.
UUNDAJI WA CLUB ZA UKIMWI;
Jumla ya club 9 za shule za sekondari zimeundwa na kupatiwa mafunzo ya kujitambua na kujilinda na magonjwa ya ngono na UKIMWI.Shule hizo ni Malinyi,Ngoheranga,Itete,Biro pamoja na Sofi kwa Wilaya ya Malinyi na kwa Wilaya ya Ulanga ni Iragua,Kichangani,Kwiro pamoja na Ulanga.4
Shule 9 ambazo zimeunda club za UKIMWI zimepatiwa vifaa vya michezo ambavyo ni mpira wa miguu na mikono.Hayo yote ni katika kupambana na hisia kali za kufanya ngono na badala yake kuhamasishwa kufanya mazoezi.
Vyakula vyenye thamani ya Tsh.4,000,000 vimenunuliwa na kugawanywa katika vituo 2 vya kulelea watoto Yatima vya Ukwama kilichopo Wilaya ya Ulanga na St.Joseph{Itete}kilichopo wilaya ya Malinyi.
Ni wajibu wa kila mwananchi,Serilakali na Wadau mbalimbali kuweka kipaumbele zaidi katika mapambano dhidi ya UKIMWI ili kuweza kupunguza na hatimaye kutokomeza janga hili.
Ulanga bila maambukizi mapya,unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana,Tutimize wajibu wetu.