Redio Ulanga ni redio ya jamii iliyoanzishwa Desemba 2010 na Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga. Redio hii ilianza kurusha matangazo rasmi mnamo Desemba mwaka 2011. Redio Ulanga Fm inasikilizwa katika umbali wa Kilomita 24,560 za wilaya na inapatikana katika mawimbi ya 91.5
Redio Ulanga ilipewa Leseni ya kurusha matangazo na mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Novemba 2011.
Katika Mkoa wa Morogoro, Redio Ulanga ni Redio ya pili kuanzishwa na Halmashauri za mkoa wa Morogoro. Lengo la uanzishaji wa Redio Ulanga ni kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi ikizingatiwa hakuna redio nyingine inayosikika inayochangiwa na jiografia ambayo ni mwinuko wa mita 1500 usawa kutoka usawa wabahari.
Redio Ulanga inasikika umbali wa Kilomita 24,560 za Wilaya ya Ulanga, pia inasikika katika maeneo mengine nje ya Wilaya ya Ulanga kama vile Wilaya za Kilosa, Liwale, Kilombero, Namtumbo, Chunya, Kyera na Kilolo.
2.0 MTAZAMO
Halmashauri ya Wilaya imejiweka yenyewe katika kutoa huduma bora kwa watu wake kwa kuwawezesha katika kuongeza kipato, kupata makazi mazuri na kuwa na maendeleo endelevu.
2.3 KUANZISHWA KWA REDIO ULANGA FM
Ulanga Fm Redio ilianzishwa kwa dhumuni kubwa la;
Kuleta chachu ya maendeleo kwa watu kuhusu mambo mbalimbali kamaafya,kilimo na mazingira.
Kuburudisha wananchi
Kuihabarisha jamii na juu ya habari na matukio mbalimbali ya kilasiku ya kitaifa na kimataifa
Kuelimisha jamii ya wakazi na wilaya za jirani
MWISHO
Kwa kipindi cha miaka mitano Redio Ulanga imeweza kujipatia wasikilizaji wengi kutokana na vipindi vyake kama vinavyooneshwa kwenye ratiba