HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA
IDARA YA MAJI
1.0 UTANGULIZI
Idara ya maji ni moja kati ya Idara 12 za Halmashauri ya Ulanga na ilianzishwa rasmi tangu serikali ilipoamua kurudisha madaraka na majukumu katika ngazi ya Serikali za Mitaa mwaka 1984.
2. Hali ya watumishi
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga katika idara ya maji ina jumla ya watumishi 8 kati ya watumishi 28 wanaohitajika kulingana na mapendekezo ya Wizara ya Maji. Watumishi waliopo wako katika maeneo mawili ambayo ni Idara ya Huduma ya maji Kijamii na Idara ya Huduma ya Maji Kibiashara;
Huduma ya maji Kijamii
Na
|
Watumishi/kundi
|
Ngazi ya elimu
|
Idadi
|
1
|
Mhandisi wa maji
|
Degree
|
1
|
2
|
Fundi sanifu
|
Form IV
|
1
|
3
|
Fundi sanifu
|
Diploma
|
1
|
4
|
Fundi sanifu wasaidizi ngazi ya Trade test
|
STV VII ( trade test)
|
1
|
|
|
Jumla
|
4
|
Huduma ya Maji Kibiashara
Na
|
Watumishi/kundi
|
Ngazi ya elimu
|
Idadi
|
1
|
Fundi sanifu
|
Form IV
|
1
|
2
|
Fundi sanifu wasaidizi ngazi ya Trade test
|
STV VII ( trade test)
|
3
|
|
|
Jumla
|
4
|
3.0 HALI YA HUDUMA YA MAJI
Miongozo na sera mbalimbali
Usimamizi na mipango yote ya utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi inazingatia misingi muhimu ifuatayo.
· Sera ya Taifa ya maji 2002.
· Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.
· Malengo ya Milenia.
· Ilani ya uchaguzi chama Tawala (CCM) 2015
· Miongozo mbalimbali inayotolewa na serikali kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo.
· Mkakati wa kupunguza umaskini na kukuza uchumi (MKUKUTA).
3.1 VYANZO VYA MAJI
Wilaya Ulanga inahudumia Wananchi maji kutoka kwenye vyanzo vya maji ambavyo hutokana na Mito, chemichemi na visima virefu.
Hali ya mazingira ya vyanzo vya maji bado ni ya kuridhisha kwani vyanzo vyote bado vinaendelea kutoa maji japokuwa kuna changamoto ya kupungua kwa baadhi ya vyanzo kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi.
3.2 HALI YA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI
Hali ya upatikanaji wa maji kwa wingi na ubora katika wilaya ni ya wastani ambapo huduma inapatikana kwa kiwango cha asilimia 59 ya wakazi wake .Aidha kuna visima vifupi vya maji vipatavyo 285, visima virefu 12 na skimu 9 za maji ya bomba zinazoendeshwa na kumilikiwa na wananchi kupitia Jumuiya za Watumiaji Maji na Bodi ya maji.
3.3 UBORA WA MAJI
Katika kuhakikisha kuwa usalama wa maji unaendelea kuwepo ,uchunguzi wa ubora wa maji unafanyika kabla ya mradi haujajengwa. Na zoezi la kutibu maji hufanyika kabla ya kugawa maji kwa kutumia madawa aina ya clorine.
3.4 USHIRIKIANO NA WADAU WENGINE WA MAENDELEO
Ili kuongeza kiwango cha utoaji na upatikanaji wa huduma ya maji Halmashauri kupitia idara yake ya maji inashirikiana na wadau wengine vizuri kama Shirika lisilo la kiserikali la Solidermed, Kanisa Katoliki Jimbo la Mahenge(CARITAS) na Lions Pure Water katika kutoa huduma kupitia miradi ya maji na kutoa mafunzo kwa wananchi.
4.0 MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI YA KATIKA 10(WSDP)
Halmashauri ya wilaya ya Ulanga inatekeleza programu ya maendeleo ya sekta ya maji katika vijiji 10 (Mgolo, Minepa, Igota/Kichangani, Nkongo, Gombe, Tanga, Ngoheranga, Lupunga, Marinyi, Kipingo na Makerere. Miradi hii inatekelezwa kwa awamu mbili. Awamu hizo ni
i) Usanifu na upembuzi wa miradi
ii) Ujenzi wa miundombinu ya maji
4.1 USANIFU WA MIRADI
Kazi ya awali katika miradi hii ilikuwa kufanya usanifu wa miradi. Aidha usanifu huu ulikuwa unategemea upatikanaji wa vyanzo vya maji kwa maeneo husika. Aina mbili ya vyanzo vya maji zilipendekezwa kutumika na wananchi kutegemea na upatikanaji wa maji kwa maeneo husika na uwezo wa wananchi katika kuendesha miradi hiyo.
Vyanzo vya maji hivyo ni :-
i) Maji ya juu ya ardhi (Mito chemchemi , mabwawa nk)
ii) Maji chini ya ardhi (Visima virefu vya maji ) au visima vifupi
4.2 MAJI YA MTO
Baadhi ya Vijiji vilichagua teknologia ya kutumia maji juu ya ardhi kwa vile kulikuwa na uwezekano wa kupata vyanzo vya maji juu ya ardhi .Vijiji vilivyochagua kutumia maji ya mto kutokana na vijiji hivyo kuwa karibu na mito ni Mgolo ,Gombe , Malinyi,Kipingo na Makerere.
4.3 VISIMA VIREFU
Katika maeneo ambayo yaliyobainika kutokuwa vyanzo vya maji ya Mito ilipendekezwa kutumika visima virefu au vifupi.
Vijiji vya Nkongo, Gombe, Kichangani, Lupiro, Minepa, Ngoheranga na Lupunga wananchi walichagua kutumia visima virefu.
Vijiji vya Kichangani, Lupiro, Minepa na Lupunga vilifaulu kwa kupata maji na ujenzi wa miundombinu ulijengwa. Vijiji vya Nkongo, Ngoheranga na Tanga vilikoswa maji, hivyo pakafanyika utafiti wa kuchimba visima virefu kwa kila kitongoji ili kuangalia uwezekano mara ya pili badala ya mradi wa maji ya bomba.
4.4 UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJI
Ujenzi wa miundombinu ya maji ipo kwenye hatua mbalimbali ikiwemo kukamilika, umaliziaji na ujenzi
A. MIRADI ILIYOKAMILIKA NA HUDUMA INATOLEWA
Miradi iliyokamilika ni Lupunga, Lupiro, Igota/Kichangani na Mgolo. Ambapo miradi yote inaendeshwa na wananchi wenyewe kwa kusimamiwa Jumuiya ya Watumiaji Maji iliyosajiriwa.
Mapungufu mbalimbali ya miradi Halmashauri, mkandarasi mshauri na Mkandarasi wa ujenzi na Bodi za maji kwa pamoja tunashughulikia kwa karibu kuzikamirisha.
B. MIRADI AMBAYO IPO HATUA YA UMALIZIAJI
Mradi ambayo ipo kwenye hatua ya umaliziaji na huduma haijaanza tolewa ni mradi wa Kijiji cha Minepa, ambapo tatizo lilikuwa bomba kupasuka karibu na mtambo wa kusukumia maji. Tatizo hili limetatuliwa na sasa upo kwenye utaratibu wa kukaguliwa na kukabidhiwa wananchi
Mradi wa pili ni Gombe ambapo chanzo ni mto, maji yalishindwa kuingia kwenye tanki. Huduma ya maji ilikuwa inatolewa bila kuingia kwenye tanki. Ila kwa sasa kunaitilafu ambapo mkandarasi yupo eneo la ujenzi anarekebisha/anakarabati. Utatuzi wa kudumu tumemuomba Katibu Mkuu Wizara ya Maji atume mtaalam tushirikiane kupitia usanifu.
C. MIRADI AMBAYO IPO HATUA YA AWALI
Miradi ambayo ipo hatua ya awali ni mradi wa maji ya bomba Marinyi, Kipingo na Makerere. Mradi wa pili ni wa uchimbaji wa visima virefu 20 Nkongo, Ngoheranga na Tanga. Ambapo wakandarasi wapo eneo la mradi wanaendelea na ujenzi.
3.5 GHARAMA ZA MRADI
Jumla ya gharama yote ya mradi wa maji ya Vijiji 10 ni Tsh 5,107,070,266.31 ambapo kiasi cha Tsh 2,164,246,008 kimepokelewa na Kimelipwa wakandarasi. Mchanganuo kwa kila mradi kama ifuatavyo;
Kijiji
|
Gharama ya Mkataba (Bila VAT)
|
KIASI KILICHOLIPWA (Tshs)
|
Kichangani
|
427,864,721.00 |
384,910,338 |
Igota
|
||
Lupiro
|
396,802,107.70 |
362,612,542. |
Gombe
|
368,431,894 |
348,381,699.18 |
Makerere
|
2,681,979,857.83 |
402,296,978.67 |
Kipingo
|
||
Marinyi
|
||
Lupunga
|
149,318,982.00 |
126,431,856.76 |
Minepa
|
378,566,952.00 |
283,503,820.02 |
Mgolo
|
147405,751.78 |
147,405,751.78 |
Mkandarasi Mshauri
|
556,700,000 |
341,000,000 |
Jumla kuu
|
5,107,070,266.31 |
2,396,542,986 |
5.0 USAJILI WA VYOMBO HURU VYA WATUMIAJI MAJI (COWSOs)
Kulingana na sheria mpya ya maji ya mwaka 2009 miradi yote ya maji inabidi iundiwe vyombo huru vya watumiaji maji vitakavyopendekezwa na kukubaliwa na jamii husika kulingana na mwongozo na sheria za maji Na. 12 ya mwaka 2009.
Katika kutekeleza jukumu hilo Halmashauri imesha sajili Jumuiya za watumiaji maji 6 ambazo
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.