SURA NA TASWIRA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA
Utangulizi
Halmashauri ya Ulanga ni mojawapo ya Halmashauri 9 za Mkoa wa Morogoro, ambazo ni Ulanga,Mvomero, Manispaa Morogoro, Morogoro,Gairo,Kilosa, Kilombero,Mji Ifakara na Malinyi.
Wakazi wa Halmashauri ya Ulanga ni mchanganyiko wa makabila mbalimbali. Kabila ambalo ni wenyeji wa Halmashauri hii ni Wapogoro. Kasi ya kupanuka kwa Halmashauri ya Ulanga imeongezeka kutokana na fursa mbalimbali zilizopo kijiografia, kiuchumi na kimazingira, jitihada zinafanyika kupitia Halmashauri na Wadau mbalimbali kuendeleza wilaya ya Ulanga katika nyanja mbalimbali ili kuleta mabadiliko ndani ya wilaya.
1.1 Mahali:
Wilaya ya Ulanga iko umbali wa Kilometa 512 kutoka Jiji la Dar es Salaam. Ipo kati ya Latitudo 4.5 Kusini na Longitudo 37.4 Mashariki. Ipo kiasi cha futi 1,600 kutoka usawa wa bahari.Ulanga inapakana na milima ya Uluguru,pia imepakana na mkoa wa Iringa,imepakana na Songea,pia imepakana na wilaya ya Malinyi na Kilombero.
1.2 Eneo:
Halmashauri ya Ulanga ina eneo la Kilometa za Mraba 14,423 sehemu kubwa ni mapori ya Hifadhi na Misitu. Sehemu kubwa ni Hifadhi ya Selous katika upande wa kusini na Mashariki na kuna Hifadhi ya Kilombero Kusini (Iluma) kwa upande wa kaskazini na Mashariki.
1.3 Hali ya Hewa
Nyanda za juu Kusini Magharibi: (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini mwa Morogoro):
Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Novemba hadi January na zinatarajiwa kuwa na mvua nyingi hadi juu ya wastani katika maeneo mengi. Hata hivyo kusini mwa mkoa wa Njombe na baadhi ya maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro (Mahenge) mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa.
Wastani wa joto ni nyuzi 180C hadi 260C wakati wa baridi (Julai– Novemb) Mvua za Vuli huanza mwezi wa Octoba hadi Februari, Mvua za Masika kuanzia mwezi marchi hadi Mei. Mvua hizo hunyesha kwa wastani wa kati ya milimita 800 hadi 1,600.
1.4 Idadi ya Watu
Wilaya ya Ulanga imekuwa ikipanuka kwa kasi kutokana na ongezeko la watu.Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Halmashauri ya wilaya ya Ulanga inawakazi wapatao 151,001 (Wanaume 75,348 na Wanawake 75,653)
Sababu inayochangia kasi kubwa ya ongezeko la idadi ya watu ni pamoja na: Kuzaliana na kuhamia. Sababu zinazochangia kasi kubwa ya kuhamia ni pamoja na :
Ongezeko la Uwekezaji wa Uchimbaji wa Mdini
Ongezeko la sehemu za biashara
Ongezeko la shughuli za kilimo na ufugaji
Uboreshaji wa miundombinu
Kupanuka kwa huduma za kijamii – mfano: shule, vituo vya afya, sehemu za starehe.
1.5 Shughuli za Kiuchumi na Ajira
Shughuli kuu zinazofanywa na wakazi waUlanga ni pamoja na:
Biashara – Jumla na reja reja
Kilimo na Mifugo –
Shughuli za ofisini
Ajira ndogo ndogo
Uchimbaji wa madini
Kilimo cha Mazao yanayolimwa nje kidogo ya Mji na katika Wilaya jirani Kilombero ni pamoja na, mpunga, mahindi, ndizi, mihogo,Viazi Vitamu, Matunda na mboga za majani.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.