ULANGA
NA FATUMA MTEMANGANI.
Zoezi la upigaji chapa mifugo wilayani ulanga mkoani morogoro limefanikiwa kwa kupiga chapa ngombe 45,771 kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili wamepiga chapa ngombe 813 .
Akizungumza na redio ulanga afisa mifugo wilaya ndg.bernard ntikabuze amesema kua jumla ya shilingi 46,584,000 zimekusanywa katika zoezi hilo la upigaji chapa mifugo.
Hata hivyo ameeleza mafanikio ya uhamasishaji wa zoezi hilo amabo ulifanyika kwa kila vijiji,kata pamoja na tarafa na kufanikisha kutengeneza vitambulisho.
Ntikabuze amesema kua mkakati uliopo kwa sasa ni kukamilisha zoezi la usajili,kuandaa orodha ya wafugaji ambao wamegoma kusajili mifugo yao ili kuwachukulia hatua za kisheria hivyo baadi ya kata wameanza kuwasilisha.
Mikakati mingine ni kuboresha nyanda za malisho,kufanya mikutano kwa lengo la kutoa elimu na hamasa juu ya uboreshaji maeneo ya malisho,kupitia upya uwekaji wa mipaka na kuwaondoa wananchi waliovamia maeneo ya malisho kwa kufanya shughuli za kilimo na makazi.
Pia kuimarisha uongozi wa wafugaji wasimamie vyema maeneo yao ya malisho,wafugaji kufanya ziara ya mafunzo juu ya uboreshaji wa nyanda za malisho,kuwawezesha wafugaji kuwa na sheria ndogo zitakazo wawezesha kusimamia maeneo yao ya malisho,kuwapeleka wafugaji kwenye ranchi za taifa kupata mafunzo na hamasa ya ufugaji pamoja na kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.