Na Fatuma Mtemangani
Ulanga
Mradi wa Land Tenia Suport Programme (LTSP) umeanza Zoezi la upimaji wa Ardhi kwa Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro katika vijiji tisa(9).
Akizungumza na Redio Ulanga Fm afisa Ardhi wilaya ya Ulanga bwana Valenc Huruma amesema kua kwa sasa wapo katika zoezi la kupima mashamba ya wananchi na wamefanikiwa kupima mashamba elfu moja na mia moja.
Bwana Huruma ameongeza kua baada ya kumaliza upimaji mashamba wananchi waliopimiwa mashamba yao kwa sasa wanawaandalia hati za umilikishwaji wa Ardhi na kukabidhiwa.
Mradi huo ni wa miaka mitatu kwa Tanzania ambapo kwa Mkoa wa Morogoro umeanza katika wilaya 3 ikiwemo wilaya ya Ualnga,Kilombero pamoja na Malinyi hivyo wilaya ya Ulanga imekua wilaya ya mfano kwa kuanza zoezi hilo.
Pia Wilaya ya Ulanga ina mipango ya kuandaa matumizi bora ya Ardhi ya vijiji na tayari vijiji vinane(8) vimeandaliwa kwa kupitia mradi huo,Lengo ni kila mwananchi anamilikishwa kipande chake cha Ardhi na kuondokana na migogoro ya Ardhi isiyo ya lazima ambayo imekua kero kubwa kwa nchini Tanzania.
Vijiji ambavyo mradi huo unawaandalia mipango ni pamoja na kijiji cha Mzelezi,Libenaga,ruaha,Mtukula,ChikweraGombe,Nkonko,Euga na Ebuyu.
Aidha amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye maeneo yaoili kila mtu aweze kunufaika na fursa hii kama wilaya na taifa kwa ujumla kwa kuondoa migogoro iliyo kwenye maeneo yao ili mradi ukifika vikwa zo viwe vimeondolewa ili kila mtu apimiwe kipande chake cha Ardhi kinachogharamiwa na serikali.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.