Na Yuster Sengo
Wananchi wilayani Ulanga mkoani Morogoro wametakiwa kuwa wa zalendo katika majitoleo kwenye miradi mbali mbali ya fedha zinazotolewa na serikali ili miradi hiyo iweze kumalizika kwa wakati
Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya fedha ,uchumi na mipango,mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga Mh.Furaha Fadhili LIlongeli amesema kuwa ni vizuri wananchi washirikishwe kwenye miradi ya maendeleo ili kusaidia kumaliza miradi hiyo kwa wakati na kwa fedha zilizopangwa
“wananchi wakishirikishwa kwenye miradi ya maendeleo itasaidia kupunguza bajeti,maana yake zile pesa kidogo zilizotufikia zikitumika vizuri pamoja na nguvu kazi miradi hii itaisha kwa wakati na kwa asilimia zote bila kuomba kuongezewa pesa nyingine” amesema Lilongeli
Aidha ameongeza kuwa kuna baadhi ya kata wananchi wanajitolea nguvu kazi na sehemu nyingine hawajitolei kabisa hali ambayo inasikitisha na pia kuvunja moyo kata zinazo jitolea nguvu kazi
“kuna maeneo mengine watu wanatoka jasho sana kwa kujitolea,lakini maeneo mengine watu hawafanyi chochote,tunasikitishwa sana kwa nguvu za wananchi kutotumika katika maeneo hayo,hivyo kamati hii ya fedha tunaomba kusisitiza kwanmba nguvu za wananchi zitumike,tusitumie tu pesa ya serikali bila kushirikisha nguvu kazi katika aeneo yetu” amesema Lilongeli
Hata hivyo Lilongeli ameongeza kuwa kwa sehemu ambazo vifaa kama cement vimepelekwa na havijatumika basi vifaa hivyo vitahamishiwa sehemu nyingine kwenye uhitaji
“katika yale maeneo tumepeleka cement hazijatumika,tunaweka maazimio hapa na tutaenda kujadili kwenye kamati .cement zile tutazihamisha kuliko kuganda pale na sisi tukapata hoja ya ukaguzi hilo jambo halikubaliki,kwahiyo kama mmeshindwa kutumia hizo cement tutazihamisha na kuzipeleka kwa wahitaji” amesema Lilongeli
Hata hivyo amewataka viongozi wa kata na vijiji kufanya uhamasishaji wa kutosha wa nguvu kazi kwani wananchi wapo chini yao na wakihamasika zaidi wanaweza kufanya kazi na kumaliza miradi kwa wakati.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.