Ulanga
na Fatuma Mtemangani
Zoezi la utoaji wa hati miliki za kimila kwa wilaya ya ulanga mkoani morogoro linaendela katika vijiji mbalambali ikiwemo kijiji cha mzelezi na kichangani.
Akizungumzia uotaji wa hati hizo afisa ardhi wilaya ya ulanga bwana valenc huruma amesema kua mpaka sasa mashamba takribani elfu kumi na moja na mia mbili yameshapimwa kwa maandalizi ya hati na utoaji wa hati hizo kwa wananchi.
Bwana huruma ameongeza kua hati hizo zinasaidia kuondoa migogoro ya ardhi,kuongeza ulinzi wa miliki za mashamba yao na kutumika kama dhamana kwenye vyombo vya fedha yaani kupata mikopo bila kizuizi chochote.
Hata hivyo zoezi hilo linaendelea katika tarafa ya mwaya katika kata ya lukande ambapo hati mia tisa tisini na tisa zimeshaandaliwa na hati mia tatu kwa ajili ya kijiji cha gombe pamoja na kijiji cha chikwera ambapo wananchi watasaini hati hizo na kukabidhiwa na kukabidhiwa rasmi.
Katika dhana nzima wa umilikshaji ardhi kwa sasa upimaji wa mashamba unaendela katika kjiji cha ikungua pamoja na idunda hivyo wananchi wamejiandaa na zoezi hilo huku kijiji cha nakafulu kuna zoezi la kupanga makazi yao kwa kutenganisha maeneo ikiwemo eneo la makazi,eneo la mashamba,eneo la misitu pamoja na malisho kwa vijiji ambavyo vina fursa ya wafugaji.
Aidha amewaomba wananchi wa vijiji ambavyo zoezi la upimaji linaendelea kutoingiza mabo ya siasa katika zoezi hilo na badala yake watoe ushirikiano kwa wataalamu walioko kwenye vijiji husika kwa kua mradi huu hauna lengo la kugawa ardhi bali kuhakikisha kuwa kipande cha ardhi ulichokua nacho kina rasimishwa ili mwananchi aweze kupata hati miliki ya kumsaidia ili kwa kutimiza ndoto zake.
Wilaya ya ulanga unatekeleza mradi wa umilikishaji ardhi mradi huu unafanya kazi tatu ikiwemo kazi ya kupanga matumizi bora ya adhi,kupima mashamba ya wananchi pamoja na kumilikisha ardhi kwa kutoa hati miliki kwa mashamba yaliyopimwa.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.