ULANGA
NA Fatuma Mtemangani,
Zaidi ya shilingi milioni tisa zimepatikana katika harambee iliyofanyika tarehe 7/1/2019 kwenye ukumbi wa Pauline uliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ishirini na nne kwa wilaya ya Ulanga.
Harambee hiyo ilizinduliwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk.Kebwe Steven Kebwe kwa kuchangia shilingi milioni moja na laki tano na Mwenyekiti wa Halmasahuri mh.Furaha Lilongeli kwa kuchangia shilingi laki tano ili watoto waliofaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka 2019 waende shu[e.
Katika harambee hiyo mkuu wa mkoa aliambatana na katibu tawala wa mkoa wa Morogoro ndugu Clifford Tandali hivyo alimpongeza mkuu wa wilaya ya Ulanga mh.Ngollo Malenya kwa ubunifu mkubwa aliouonyesha katika kufanikisha agizo la mkoa kuhusu ujenzi wa vyumba 24 vya madarasa.
“ Nikupongeze sana mkuu wa wilaya kwa ubunifu ulioufanya na kutekeleza maagizo ya mkoa kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa na hiyo isiwe mwisho wa kuchangia naomba iwe endelevu,lakini pia wana Ulanga msichoke kuchangia ujenzi huo kwani watoto wetu wanafanya vizuri sana katika masomo yao kwa shule za msingi na sekondari katika mkoa wa Morogoro hivyo kama mzazi unapaswa kuwa mstari wa mbele kujitoa kwenye michango na hata nguvu kazi.”
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh.Ngollo Malenya alimshukuru mkuu wa mkoa dk.Kebwe Steven Kebwe,mbunge wa jimbo la Ulanga mh.Goodluck Mlinga,waheshimiwa Madiwani,viongozi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga,viongozi wa Dini,viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wadau wote wa Maendeleokuhudhuria harambee hiyo na kuchangia pesa kwa ajili ya ujenzi huo.
Wilaya ya Ulanga inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa ishirini na nne ambavyo mpaka kufikia tarehe 28/1/2019 vinatakiwa kukamilika hivyo mkuu wa wilaya aliamua kufanya harambee hiyo ili kusaidia wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kuendelea na masomo yao.
Mkuu wa wilaya alizindua harambee iliyoshirikisha wadau mbalimbali wa Maendeleo ndani na nje ya Ulanga na kufanikisha kukusanya michango vifaa vyenye thamni ya shilingi milioni tisini na tano laki tatu sitini na sita elfu[95,366,000] hivyo amewaomba wananchi wazidi kuchangia ili kufanikisha ujenzi huo.
Harambee hiyo imebeba kauili mbiu isemayo“ Umoja wetu ndiyo nguvu yetu Ulanga madarasa kwanza changia buku plus mtoto aende shule.”
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga ina jumla ya Shule za Msingi 61 zikiwemo 60 za Serikali na moja Binafsi ambazo zimefanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba na kupata nafasi ya kwanza kimkoa na kitaifa nafasi ya kumi na sita darsa na kwa darasa la nne kimkoa imeshika nafasi ya kwanza na kitaifa imeshika nafasi ya tano kwa mwaka 2018 hali iliyopelekea upungufu wa vyumba vya madarasa.
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.