ULANGA
Na
Fatuma Mtemangani
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro kupitia kikao cha Fedha,Uongozi na Mipango kimewataka watumishi wa serikali wakiwemo maafisa watendaji wa Kata,Vijiji,Tarafa na Wilaya kuacha ufisadi na kutoleta mambo ya itikadi za kisiasa na badala yake kuwa na maadili bora,na nidhamu na kujipanga kwa mwaka mpya wa serikali ili kutoa huduma nzuri kwa jamii.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro dk.Kebwe Steven Kebwe wakati alipokutana na wakuu wa Idara na watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga ikiwemo waheshimiwa madiwani katika kikao cha baraza la madiwani kilicholenga maagizo yaliyotolewa na kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa yaliyotolewa wakati wa kujadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hersabu za serikali{CAG}.
Dk. Kebwe pia amewataka watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawajibike na,kujituma kwa bidii ili kuleta maendeleo kwa wana Ulanga.
“kama wewe ni kiongozi na unategemewa na serikali kwanini ufanye kazi kwa mazoea ni lazima uwajibike kwa ajili ya maendeleo ya wana ulanga na taifa kwa ujumla,wapo watu wanakutegemea wewe kiuchumi sasa mistake tuuanze mwaka huu vibaya nasema fanyeni kazi”.
Pia amewataka Idara ya Kilimo kutoa elimu kwa vijana wapende kilimo,na kuwaingizia pesa mfuko wa wnanwake kwa wakati kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi ili kuunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh.dk.John Pombe Magufuli ya Tanzania ya viwanda kwa kutofanya hivyo ni kurudisha nyuma maendeleo kwa wananchi.
Aidha amewataka wanasheria wa serikali wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga kwa kushirikiana na viongozi husika kusimamia kesi za serikali mahakamani bila kufanya hujuma na kuacha propaganda kwa kufanya hivyo ni kutoitendea haki serikali.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.