Na Ester Kaonja
mkurugenzi wa mashitaka nchini tanzania (dpp) amewafutia kesi washkakiwa wanne wa kesi za mauaji
akisoma hati hizo za kuwafutia mashtaka mwendesha mashtaka wa polisi inspekta simoni mgonja mbele ya hakimu mfawidhi mh. james muhanus amewataja washtakiwa hao kuwa ni dotto majuakano mwenye umri wa miaka 26, pamoja na mwenzake tungu lufunga mwenye umri wa miaka 26, wenye kesi ya mauaji no.8/2018, wote ni wakazi wa mtimbira wilayani malinyi mkoani morogoro.
mwingine ni fransis peter mwanampalu mwenye umri wa miaka 44, mwenye kesi ya mauaji no. 7/2019 mkazi wa mtimbira wilayani malinyi mkoani morogoro, na fransis msahala mwenye umri wa miaka 23,mwenye kesi ya mauaji no. 5/2019 mkazi wa kijiji ruaha wilayani ulanga mkoani morogoro.
inspekta mgonja amesema kuwa washtakiwa hao wameachiliwa chini ya kifungu no 91 (1) cha sheria ya makosa ya jinai sura no.20 marejeo ya mwaka 2019 hivyo mahakama ya wilaya ya ulanga imewaachia huru washtakiwa wote kama walivyofutiwa mashktaka yao na mkurugenzi wa mashtaka nchini.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.