ULANGA
NA
Fatuma Mtemangani
Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania Tawla wamekuwa wakiwajengea uwezo Wanawake mara kwa mara kwa kuwapatia mafunzo ili waweze kujua haki ya kupata ardhi,kutumia ardhi,kumilik ardhii, na kuuza ardhi.
Kauli hiyo imetolewa na mmoja wa wanasheria wanawake bi maria mruma wakati akizunguza na viongozi wa jukwaa la wanawake kutoka kata mbalimbali walioudhuria katika mafunzo ya kuwajengea uwezo akina mama hao katika ukumbi wa Udeko kwa muda wa siku mbili tarehe 7/6/2019 hadi tarehe 8/6/2019.
Hapo awali wanawake walikuwa hawana uelewa wa kutosha juu ya umiliki wa ardhi na badala yake wanaume ndiyo walikua wakiandika majina yao wanapokwenda kulipia ardhi, hivyo wanatakiwa kufahamu haki zao hasa za umiliki wa aridhi na mirathi.
“Wanawake wezangu mna haki ya kupata ardhi,kutumia ardhi,kumilik ardhii, na kuuza ardhi lakini piamuwe makini na kujithibitishia pale mwanandoa wako amechukua mkopo kwenye taasisi ya kifedha wakati mmeweka rehani,na pia mnatakiwa kumtafuta mwanasheria wa chama cha wanasheria wanawake [TAWLA] pale unapoona mali uliyowekwa rehani inataka kuuzwa ili uweze kupata msaada kwa wakati.Alisema Maria Mruma
Wanawake wamekuwa wakifuchwa siri za wanandoa wao hali ambayo inapelekea wanandoa hao kukosa haki zao hasa kwenye mali kama vile nyumba na mashamba.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jukwaa la wanawake mkoa wa morogoro bi amina seifu mgerwa amesema kua elimu iliyotolewa na Tawla itawasaidia wanawake kujua namna ya kupata haki zao katika suala zima la kumiliki aridhi,sheria ya ndoa na haki nyingine ambazo hawazifahamu ili kuondoa dhana ya kujiona wanawake wananyanyasika.
Aidha baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo bi Habiba Njaa pamoja na bi Hawa Mgaichuma wamewashukuru Tawla kwa mafunzo wanayotoa na kuwaomba kuendelea kupeleka elimu hiyo katika vijiji vyote wilayani ulanga ili kuwasaidia wanawake ambao hajatambua haki zao waweze kuzielewa kwani itapunguza malalamiko yanayotokana na uelewa mdogo wa sheria miongoni mwao.
Kwa wilaya ya Ulanga mradi wa urasimishaji Ardhi umelenga kufikia vijiji 52 kwa wilaya ya Ulanga hivyo mpaka sasa tayari mradi umefanya kazi katika vijiji 40 bado vijiji 12 hii ni kutokana na changamoto ya mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha wilayani Ulanga kuharibu miundombinu ya barabara na mashamba kujaa maji hali iliyosababisha kusimama kwa zoezi la upimaji wa mashamba katika vijiji vilivyosalia.
Baadhi ya wananchi wameelezea uhalisia wa mradi huo ulivyowasaidia wanawake kuwa na hati miliki za kimila kwa kuwainua wanawake kiuchumi kupitia Ardhi zao wenyewe kwenye ndoa zao na hata famila ya wazazi wake.
Mradi wa urasimishaji wa Ardhi,Land Tenure Support Programme [LTSP] kwa wilaya ya Ulanga unatarajia kukamilika tarehe 30/6/2019 hivyo zoezi la upumaji litaendelea kwa vijiji 12 vilivyobaki mpaka mradi utakpokamilika kwa wakati
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.