ULANGA
NA FATUMA MTEMANGANI
Wanawake wa wilaya ya ulanga mkoa morogoro wameshauriwa kuudhuria mafunzo mbalimbali yanatolewa na chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania Tawla ili waweze kufahamu haki zao hasa za umiliki wa Aridhi na Mirathi
Kauli hiyo imetolewa na mmoja wa wanasheria wanawake bi Maria Mruma wakati akizunguza na viongozi wa Jukwaa la Wanawake kutoka kata mbalimbali walioudhuria katika mafunzo hayo lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kutambua haki zao.
Hapo awali Wanawake walikuwa hawana uelewa wa kutosha juu ya umiliki wa Ardhi na badala yake Wanaume ndiyo walikua wakiandika majina yaoa wanapokwenda kulipia Ardhi, hivyo Halmasahuri kwa kushirikiana na chama cha Wanasheria cha Wanawake TAWLA wamekuwa wakiwajengea uwezo mara kwa mara kwa kuwapatia mafunzo ili waweze kujua haki ya kupata Ardhi,kutumia Ardhi,kumilik Ardhii, na kuuza Ardhi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jukwaa la wanawake mkoa wa morogoro bi amina Seifu Mgerwa ndiyo mgeni rasmi katika mafunzo hayo amesema kua elimu iliyotolewa na TAWLA inawasaidia Wanawake kujua namna ya kupata haki zao katika suala zima la kumiliki Aridhi,Sheria ya ndoa na haki nyingine ambazo hawazifahamu ili kuondoa dhana ya kujiona wananyanyasika.
Aidha baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo Bi Habiba Njaa pamoja na Bi Rehema Athumani wamewashukuru TAWLA kwa mafunzo wanayotoa na kuwaomba kuendelea kupeleka elimu hiyo katika vijiji vyote Wilayani Ulanga ili kuwasaidia Wanawake ambao hajatambua haki zao waweze kuzielewa kwani itapunguza malalamiko yanayotokana na uelewa mdogo wa sheria miongoni mwao.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.