Yuster Sengo mwenge
Wananchi wilayani ulanga mkoani morogoro wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa covid 19 kwa kuepuka misongamano ,kuvaa barakoa na kunawa mara kwa mara kwa kutumia vitakasa mikono.
Haya yamesemwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru maalumu luten JOSEPHINE MWAMPASHI wakati akitoa ujumbe wa mwenge katika kijiji cha kivukoni wilayani ulanga mara baada ya kukabidhiwa kutoka wilaya ya kilosa
Lutein mwampashi amesema kuwa kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu TEHAMA NI MSINGI WA WA TAIFA ENDELEVU ITUMIE KWA USAHII NA UAJIBIKAJI.
Sambamba na hayo kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru amesema kuwa ‘‘tehama ni nyenzo muhimu na ya kisasa katika kuchochea maendeleo , teknologia hii inayotumia njia mbalimbali kama vile kubeba, kusafirisha,kuchakata, pamoja na kulinda taarifa mbalimbali takwimu, sauti pamoja na picha kwa kutumia njia za mawasiliano kama vile simu za mkononi, compyuta ,televisheni, redio na mashine mbalimbali zinazotumika kutuma au kupokea taarifa mbalimbali za kifedha``
Aidha luten mwampashi pia ameelezea umuhimu wa kutumia teknogia kwa watanzania kwa kutokana na uwepo wa teknologia ya habari na mawasiliano umerahisisha mfumo mzima wa elimu kwa wanafunzi kujifunza kwa kutumia picha na sauti na kuongeza weledi na ufanisi katika kujifunza kwao.
Hata hivyo mwenge mwenge wa uhuru umezindua miradi sita ikiwemo mradi wa vijana nguvu kazi seremala mbasa, mradi wa maji igumbiro, mradi wa shule ya msingi mavimba B, mradi wa kitalo cha miche ya mitiki mavimba, mradi wa kuongeza thamani ya zao la mpunga kijiji cha mbuyuni, mradi wa zahanati kijiji cha minepa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya ulanga mh. Ngolo Malenya amesema kuwa kazi ya serekali ni kutekeleza irani ya chama na kusogeza huduma kwa wananchi, hivyo amemshukuru kiongozi wa mbio za mwenge kwa kukagua na kuzindua miradi mbalimbali katika wilaya hiyo.
Pia luten mwampashi ametoa wito kwa halmashauri kuweka pesa kwenye akaunti za kijiji kwa ile miradi inayotekelezwa kwenye ngazi za kijiji ili wazisimamie wenyewe kwani wana viongozi ambao wanaweza kusaidiana katika kukamilisha miradi yao ya kimaendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.