Na Ester Mwita
Wananchi wameombwa kujitolea katika kutekeleza wa miradi kwa ushirikiano na serikali ili iweze kukamilika kwa wakati na kutoa huduma kwa haraka
Kauli hiyo ilitolewa na mchumi kutoka idara ya mipango wa halmashauri ya wilaya ya ulanga bw. deogratius lihengelimo wakati akizungumza na radio ulanga fm wakati akizungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya halmashauri
Alisema miradi inakosa ushirikiano kutoka kwa wananchi inatumia mda mrefu kukamilika na halimashauri inatumia gharama kubwa katika kuikamilisha
”wananchi wanaposhiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali mbali kazi inakuwa ni rahisi na inakamilika kwa mda uliopangwa”alisema lihengelimo
Alise ma katika kutekeleza miradi hiyo halmashauri imetenga zaidi ya shiling milioni miatatu kwa ajili ya ukarabati wa visima 4 na uchimbaji wa visima 80 vya kati vijiji 20 ikiwemo mawasiliano na kijiji cha mwaya .
“Uchimbaji wa visima80 vya kati katika vijiji 20 vinajumuisha vijiji vya mponera,mawasiliano ,ikungua,mbuyuni,na chikuti wakati ukarabati wa mradi wa maji wa mwamchili unajumuisha vjiji vya ruaha ,mzelezi,chirombola ,na mwaya” alisema
Pia itatekeleza ukarabati wa mradi maji wa mwamchili utakaojumhisha vijiji ya ruaha na mzelezi ambao ukikamilika tatizo la maji litapingua kwa kiasi kikubwa
Aidha kwa mwaka wa fedha uliokamilika wa mwaka 2017/2018 wanaendelea na ukamilishaji wa uchimbaji wa visima 27 na tayari visima 24 vimechimbwa na ufungaji wa pampu unaendelea katika uchimbaji huo visima vitatu vimekosa maji katika vijiji vya igumbilo,mavimba,milola,ikungu,na luhombelo mradi ulighalimu milioni mia nane na tatu lakimoja sabini na sita elfu na sitini na nne 803,176,064.
Aidha alisema wanaendelea na ukarabati wa miundombinu ya maji mahenge mjini kwa usimamizi wa moruwa mabomba mia 6000 yamelazwa na dira 450 zimepokelewa na kuanza kufungwa kwa wateja .
“Tumetandaza mambomba mita 6000 na dira mianne hamsini 450 tayari zimepokelewa na kufungwa kwa wateja ulighalimu milioni mia natatu lakitisa na tisa elfu mia tisa sabini nne 103,909,974 “ alisema rwengelimo
Katika sekta ya afya kwa mwaka wa fedha 2018/2019 halimashauri imetenga milioni ishirini kwa ajili ya ukarabati wa wodi ya wanaume katika hosipitali ya ulanga iliyopo mjini mahenge
“Tumenga shilingi milion ishirini 20,000,000. kwa ajili ya ukarabati wa wodi ya wanaume katika hosipitali ya wilaya “
Na kwa mwaka wa fedha uliomalizika halmashauri inaendelea kukamilisha ujenzi na ukarabati wa kituocha afya cha lupiro thearter,labour,nyumba ya mganga,mortuary katika kata ya lupiro ulioghalimu shiling milion mia nne 400,000,000.
Tunajenga wodi ya akina mama katika hospitali ya wilaya ulioghalimu milionio hamsini 50,000,000 na ujenzi wa jengo la kujisubilia akina mama katiak kituo cha afya cha mwaya ulioghalimu milioni thelathini na sita laki tisa na sitina na nane elfu 36,968,000 alisema liengelimo.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.