ULANGA
NA FATUMA MTEMANGANI
Wanainchi wa wilaya ya ulanga mkoani morogoro wameaswa kuchukua taadhari juu ya ugonjwa wa kipindupindu katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha wilayani ulanga.
Hayo yameelezwa na afisa afya wilaya ya ulanga bw. samson mweta wakati akizungumza na redio ulanga fma ofisini kwake akielezea juu ya mikakati ya serikali katika kupambana na magonjwa ya milipuko hususani katika kipindi hiki cha mvua za vuli.
Hata hivyo bw.mweta amesisitiza mambo matatu katika kujikinga na ugonjwa huo jambo ikiwemo kila mwanainchi kuhakikisha anakuwa na choo kilichokuwa bora na kinachotumika,kuchemsha maji safi na salama ya kunywa, na kunawa mikono kwa sabuni hasa baada ya kutoka chooni na kabla ya kabla ya kula kitu chochote.
Aidha ametoa tahadhari kwa mtu yeyote ambaye atahisi kuharisha au kutapika ni vema afike haraka katika zahanati iliyo karibu, ofisi za vijiji, au wahudumu wa afya ilikujua tatizo kama ni la kipindupindi.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.