ULANGA
NA FATUMA MTEMANGANI
Mradi wa urasimishaji wa Ardhi,Land Tenure Support Programme [LTSP] umeleta mafanikio kwa kuleta mpango wa matumizi bora ya Ardhi kwa kutenga maeneo ya kijamii,upimaji wa mashamba,kujenga uelewa wa masuala ya Ardhi kwa wananchi wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.
Akizungumza katika mdahalo wa uhalisia wa mradi huo afisa Ardhi wa wilaya ya Ulanga bwana Vallenc Huruma amesema kuwa,mradi huo pia umeondoa migogoro baina ya wakulima na wafugaji,wakulima na Hifadhi ya Selous,kijiji na kijiji,wakulima kwa wakulima pamoja na kijiji na wananchi.
Bwana Vallenc aliongeza kuwa mradi pia umesaidia kuongeza thamani ya Ardhi ikiwemo uuzwaji holela wa Ardhi pamoja na jamii kutoharibu vyanzo vya maji kwa kufuata sheria mama ya mazingira na kuhifadhi misitu ya vizuri,kufanya usafi na ulinzi kwenye misitu yao ya vijiji,kwani dhima ya serikali kwenye hati miliki ya kimila ni mwananchi kujua miliki ya kipande chake cha Ardhi na kumuondolea migogoro ya mipaka baina yake na jirani yake.
“Migogoro ya Ardhi kwa sasa wilaya ya Ulanga imepungua kabisa hasa kwa jamii ya wafugaji tofauti na hapo awali ambapo ofisi yangu ilikuwa ikipokea kesi nyingi lakini kwa sasa hakuna kesi yeyote inayoletwa kwenye ofis yangu na pia jamii imeelimika juu ya matumizi bora ya Ardhi kwa kutenga maeneno ya makazi,makaburi,shule,ofisi za vijiji,Taasisi,eneo la malisho na kilimo”.Alisema Vallenc Huruma
Pia mradi umewajengea uwezo vyombo vya utatuzi wa migogoro ya Ardhi ikiwemo mabaraza ya Ardhi ya vijiji na mabaraza ya kata kwa wilaya ya Ulanga,pia kuwajengea uwezo misaada ya kisheria kwa wanawake kujua haki ya kumiliki Ardhi kupata mirathi ya Ardhi kwa mume wake hata kwa familia ya wazazi wake kupitia chama cha sheria cha wanawake Tanzani [TAWLA].
“kwanza nawashukuru sana wananchi hao kutambua nini maana ya mradi na unafanya nini katika vijiji vyao,kwa uelewa huo naamini mpango wa matumizi bora ya Ardhi utafanyia kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa”Alisema Vallenc.
Aidha umesaidia kukarabati ofisi za masijala ya Ardhi,umeshawishi wa kujengwa baraza la Ardhi la wilaya na umeanza rasmi kwa uwekaji wa alama na upimaji unaotumika ni kupima kwa kutumia teknolojia rafiki kabisa hivyo ameataka wananchi wasiopima mashamba yao kwenye maeneo yao kwani mradi ukimaliza muda wake mwananchi atapimiwa kwa gharama yake.
Kwa wilaya ya Ulanga mradi wa urasimishaji Ardhi umelenga kufikia vijiji 52 kwa wilaya ya Ulanga hivyo mpaka sasa tayari mradi umefanya kazi katika vijiji 40 bado vijiji 12 hii ni kutokana na changamoto ya mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha wilayani Ulanga kuharibu miundombinu ya barabara na mashamba kujaa maji hali iliyosababisha kusimama kwa zoezi la upimaji wa mashamba katika vijiji vilivyosalia.
Baadhi ya wananchi wameelezea uhalisia wa mradi huo ulivyowasaidia wanawake kuwa na hati miliki za kimila kwa kuwainua wanawake kiuchumi kupitia Ardhi zao wenyewe kwenye ndoa zao na hata family ya wazazi wake.
Wananchi hao wameiomba ofisi ya Ardhi kuwaongezea thamani ya hati miliki ya kimila lengo likiwa ni kujikwamua kiuchumi,na mradi utapoisha wataalam wa LTSP waongezewe muda wa kubaki Ulanga kuwasidia wananchi kusimamia kupima maeneo yaliyobaki ili kusiwe na migogoro inayowahusu wananchi.
Mradi wa urasimishaji wa Ardhi,Land Tenure Support Programme [LTSP] kwa wilaya ya Ulanga unatarajia kukamilika tarehe 30/6/2019 hivyo zoezi la upumaji litaendelea kwa vijiji 12 vilivyobaki mpaka mradi utakpokamilika kwa wakati
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.