Na . Yuster Sengo
Wakulima wameshauriwa kutengeneza na kuandaa jokofu la asili kwaajili ya kutunzia mazao yao ili yasiharibike wakati wakiwa wanatafuta soko la kuuza mazao hayo
Ushauri huo umetolewa na Afisa wa jeshi la kujenga Taifa (JKT) bw.Rafii Rajab wakati akizungumza na redio Ulanga fm kwenye banda la JKT wakati wa maonesho ya nanenane kanda ya mashariki yanayofanyika mjini Morogoro 2023
Aidha ameongeza kuwa utaalam uliotumika kwenye kutengeneza jokofu hilo la asili ni wakawaida ambapo mtu yoyote anaweza kulitengeneza kwa matumizi ya nyumbani
“hapa unatumia miundombinu mbalimbali kama makuti,mkaa,mbao na waya lengo kubwa ni kuhifadhia mboga mboga ili zisiharibike lakini pia vinywaji ili viweze kupata baridi “Amesema Bw.Rajab
Hata hivyo ameongeza kuwa ili kuweza kupata ubaridi mzuri kutoka kwenye jokofu hilo inakulazimu kumwagilia maji ya kutosha kwenye mkaa kwa siku mara tatu hadi nne
“tukimwagia mkaa wetu maji kwa siku mara tatu kinachotokea ndani ya jokofu letu ni ubaridi na vile vitu vinavyopatikana humo ndani vinapata ubaridi unaosaidia kufanya vitu hivyo kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika”Ameongeza Bw.Rajab
Maonesho ya nane nane yanafanyika mjini Morogoro kwa kanda ya mashariki inayobebwa na kauli mbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula”
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.