Na . Yuster Sengo
Wakazi wa wilaya ya Ulanga mkoani morogoro wametakiwa kutumia soko kuu la Mahenge mjini lililoanza kutumika 17 july 2020 kwaajili ya kuuza bidhaa zao
Akizungumza wakati akisimamia zoezi la wafanyabiashara kuhamia katika soko hilo afisa biashara wilaya ya ulanga bi Jasmin Mlyandi amesema kuwa soko hilo jipya limeanza kutumika rasmi na wafanyabiashara wadogowadogo wote wanatakiwa kutumia soko hilo kwa ajili ya kufanya biashara zao
Aidha ameongeza kuwa kwa wafanyabiashara ambao walikosa maeneo wamepewa maeneo ya muda huku utaratibu mwingine ukiwa unaendelea na wafanyabiashara hao wapo kwenye hayo maeneo waliyotengewa wakiendelea na biashara zao
‘’Kwa kweli leo soko letu kuu limefunguliwa rasmi na wafanyabiashara wale wadogo wadogo wamefanikiwa kuhamia katika soko hilo jipya kwaiyo wapo tayari kufanya biashara zao wakiwa mahali salama na pa uhakika’’ alisema bi jasmin.
Lakini pia amewasihi na kuwataka wafanyabiashara wote ambao wamekaidi agizo la serikali kuhamia katika soko hilo jipya kuhamia sokoni hapo mara moja kwa kuwa ndio sehemu sahihi iliyopangwa na serikali na si pengine
Kwa upande wao wafanya biashara wadogo wadogo ambao wameshahamia katika soko hilo wameipongeza serikali kwa kuwajengea soko na kupata sehemu sahihi ya kufanya biashara bila shida yeyote
‘’mimi naipongeza serikali yetu sana tena naipa hongera kubwa sana kwa kututengenezea soko zuri la kudumu ambalo tunafanya biashara zetu vizuri siku hizi hatutanyeshewa na mvua wala kupigwa na jua tupo sehemu nzuri kabisa’’ aliongea mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo
“Tunashukuru halmashauri kwa kuweza kumalizia hili soko na leo hii tumeanza kulitumia rasmi,eneo hili ni zuri na kumechangamka sana na kunafikika kwa urahisi tofauti na kule mwanzo ambapo kama mtu ana gari hawezi kufika hadi eneo la soko na gari yake ila hapa sasa ni pazuri na barabara imechongwa vizuri hivyo kurahisishia usafiri mbali mbali kufika hapa “Ameongeza mfanyabiashara huyo
Katika kila jambo zuri hapakosi changamoto hivyo basi serikali ya halmashauri ya wilaya ya ulanga mkoani morogoro limewataka wafanya biashara wote katika soko hilo jipya kuvumilia changamoto zote ambazo zinajitokeza na kwa kushirikiana kwa pamoja wanaweza zitatua
Mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.