ULANGA
Na
Fatuma Mtemangani
Wakazi wa kijiji Mbagula kata ya Vigoi Wilaya Ulanga wametakiwa kulipia mradi wa maji kwa mwezi kwa sh.500 kwa wale wanao chota maji katika bomba hilo na kwa wale walio vuta maji ndani kwao wanatakiwa kulipia sh.5000 kwa mwezi, pia fedha ambazo zitakusanywa kwaajili ya matengenezo ya bomba.
Akizungumzia michango ya mradi huo Mwenyekiti wa Kiijji hicho ndugu Credo Joseph Mbalashi amesema kuwa katika mradi huo kunakisima kimoja ambacho kina urefu wa mita 100 ambapo kimejengewa na kuweka pampu na kina uwezo wa kutoa maji lita 3165 kwa saa moja.
Ndugu Mbalashi amewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa na umoja wa kutunza miundo mbinu ya maji katika kijiji chao kwani serikali bado wanafanya jitihada ya kuendelea kufuatilia visima vilivyo baki.
Mradi wa visima vya maji katika kijiji cha Mbagula Kata ya Vigoi Wilayani Ulanga mkoani morogoro umekamilika japo kwa kiasi na sio huku jitihada zingine za kukamilisha miundo mbinu ya maji iliyobakia zinaendelea katika kijiji hicho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.