Na Yuster Sengo
Wakazi wa kitongoji cha epanko ,wametakiwa kuacha kusikiliza maneno ya kuzusha kuhusu mradi wa uchimbaji madini ya kinywe unaotarajiwa kuanza kutekelezwa katika kijiji hicho cha epanko
Akizungumza katika kikao cha kumi cha kikosi kazi cha mradi wa uchimbaji madini ya kinywe ,katibu tawala msaidizi anayeshughulika na ardhi na miundombinu ofisi ya mkuu wa mkoa,Bw.Lucas Mwaisaka amesema kuwa mradi huo ni wa uhakika na hivi karibuni wananchi wataanza kulipwa fidia
“msisikilize watu wanaozusha kuwa mradi huu ni wa kitapeli,mradi huu ni wa kweli na wa uhakika na ndiyo maana hata ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro imenituma mimi kuja hapa kwaajili ya kuhudhuria kikao hiki ambacho ni muhimu sana “amesema Mwaikasa.
Aidha ameongeza kuwa taarifa za kikao kazi hiki zinafika hadi mkoani na katika wizaraya madini ili kufata utaratibu woteunaotakiwa
Naye msemaji wa Meneja mahusiano ya jamii wa kampuni ya Tanzagraphie Bw.Benard Mihayo ameema kuwa kukaa kimya kwa muda mrefu kwa kampuni hiyo ni kutokana na kupitiwa kwa mchakato mpana na kufata taratibu zote zinazotakiwa ili kuweza kutekelea mradhi huo kwa umakini
Aidha ameongeza kuwa suala la mwenyekiti wa kitongoji hicho kurudisha nyuma juhudi za mradi huo unafahmika hadi kwa mkuu wa mkoa hivyo amewatoa wasiwasi wakazi wa epanko kuhusu suala hilo
“suala hili la mwnyekiti linafahamika hadi mkoani,kwahiyo niwatoe wasiwasi suala hili litashughulikiwa vizuri na serikali na mradi huu utasonga mbele”
“nawaomba mbadili fikra kwa kupandikizwa na watatu wachache ambao hata hawapo kwenye eneo la mradi”ameongeza Mihayo
Kwa upande wa Bw. Justine Bundu aliyekua akimuwakilisha mwenyekiti wa kikao hicho amesema kuwa ,ni vyema wakazi wote wa epanko wakakubaliana na mradi huu kwani utaleta faida kwa mtu mmoja mmoja na halmashauri kwa ujumla
“kampuni hii itatuletea faida kubwa sana kwani kwa upande wa halmashauri mrahaba utakaokuwa unakusanya kwa mwaka utakuwa n mara mbili ya ule unaokusanywa kwasas”amesema Bundu
Mradi huu unatarajiwa kuwa wa kipindi cha miaka 23 ambapo utaleta faida mbali mbali kwa wakazi wa epankona wilaya ya ulanga kwa ujumla
Ameongeza kuwa ,kampuni isingependa wakazi wa epanko wafanyiwe tathmini kwa lazima hivyo amewataka watu hao kuwasawishi wenzao kufanya tathini kwa hiari yao
“kampuni inatamani kila mtu afanye tathmini kwa hiari yake ,lakini kama kuna baadhi ya watu wanagomea hilo basi itafika siku itabidi tathmini itafanyika kwa lazima “amesema Mihayo
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.