MBUNGE WA JIMBO LA ULANGA MKOANI MOROGORO MH. GOODLUCK MLINGA AMEZINDUA MPANGO WA MOTISHA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI WILAYANI YA ULANGA KWA LENGO LA KUWAFANYA WATUMISHI HAO WAFANYE KAZI KWA WELEDI KATIKA KUWATUMIKIA WANANCHI.
AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KATIKA UKUMBI WA PAULINE WILAYANI HAPA MH.MLINGA AMESEMA KUA MPANGO HUO UMELENGA KUBORESHA MASLAHI YA WATUMISHI KATIKA KUWAPATIA NYUMBA BORA ZA KUISHI, USAFIRI, VITENDEA KAZI KWA MASLAHI YAO BINAFSI.
AIDHA KWA UPANDE WAKE MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA NDUGU YUSUF SEMUGURUKA AMESEMA KUA LICHA YA WILAYA YA ULANGA KUWA NI MOJA KATI YA WILAYA ZILIZO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU YASIYOFIKIKA KIRAHISI LAKINI SERIKALI INAENDELEA KUJITAHIDI KUHAKIKISHA WATUMISHI WAKE WANATENGENEZEWA MAZINGIRA MAZURI YATAKAYO WAPA URAHISI WA KUFANYA KAZI.
HATA HIVYO AMEWATAKA WATUMISHI WOTE KUFANYA KAZI KWA BIDII WAKATI SERIKALI INA FANYA JITIHADA ZA KUWAWEKEA MAZINGIRA MAZURI WAKIWEMO MAAFISA UGANI.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.