ULANGA
NA Fatuma Mtemangani
Wilaya ya Ulanga ni miongoni mwa Wilaya zinazolima zao la Korosho,kilimo cha Korosho kilianza tangu kipindi cha ukoloni lakini kwa kipindi kirefu uendelezaji wa zao hili halikupewa msukumo wa kutosha hivyo ilisababisha kukosa huduma za msingi kama vile palizi,udhibiti wa magonjwa na wadudu hali iliyopelekea wengi kutelekeza mashamba ya korosho.
Akizungumzia zao hilo la korosho afisa mazao Wilayani Ulanga bwana Revocatus Ngusa alisema kuwa hadi kufikia sasa Wilaya ya Ulanga imefanikiwa kuwa na mikorosho mikubwa zaidi ya laki tana na elfu thelathini{530,000} hivyo Halmashauri imefanya jitihada ili iweze kuleta tija katika uzalishaji.
Bwana Ngusa aliongeza kua katika msimu wa mwaka 2012/2013 Wilaya ilianza utekelezaji wa mpango wa ufufuaji wa zao la korosho katika ukanda wa chini hasa kwenye tarafa za Lupiro,Vigoi,Ruaha na Mwaya kwa kushirikina na Bodi ya Korosho Tanzania na Wadau wa Maendeleo katika sekta ya Korosho kama Swisscontact Tanzania.
Hata hivyo utekelezaji wa shughuli za Maendeleo ya zao la Korosho kwa mwaka 2017/2018 Wilaya ya Ulanga ilianza kutoa huduma za ugani katika zao Korosho na Halmashauri imewezesha mafunzo ya kilimo bora cha korosho na kufanya ziara ya mafunzo mkoani Mtwara kwa vikundi vinane na wataalamu wanane kutoka vijiji vya Nakafulu,Igumbiro,Mavimba,Nanungu,Iragua,Mbuga na Minepa.
Katika kusimamia usambazaji wa pembejeo za zao la Korosho na uvunaji kwa Halmashauri na kushirikiano wa Bodi ya Korosho imewezesha usambazaji wa pembejaeo hasa mbegu za Korosho na kuzalisha miche na kugawa kwa wakulima kulingana na mahitaji ya kijiji.
“kutokana na mgao wa mbegu tulizopata msimu huu Wilaya ilizalisha miche laki moja tisini na moja elfu mia tisa ishirini na mbili kupitia vikundi,taasisi na watu binafsi saba na kugawiwa wakulima katika kata za Mbuga,Euga,LUKANDE,Ketaketa,Vigoi,Msogezi,Kichangani,Lupiro,Iragua,Milola na Minepa.
Aidha Wilaya ya Ulanga imefanikiwa kutoa Elimu ya uongezaji wa thamani kwenye zao la Korosho kwa kukuza ubanguaji na usindikaji kwa vikundi sita kwa vijiji vyaMinepa,Mavimba,Igumbilo,Nanungu,Mbuga na Nakafulu pamoja na kukuza masoko ya ndani ya zao la Korosho.
Pia wananchi wanaendelea kuhamasishwa juu ya umuhimu wa matumizi ya Korosho kama chakula muhimu kwa binaadamu ili kuhamasisha kununua Korosho hivyo wakulima wengi wamehamasika katika kilimo cha Korosho na kuongeza mahitaji ya pembejeo za korosho{Mbegu na Miche} toka wakulima 146 kwa mwaka 2012/2013 hadi wakulima 5,000 kwa msimu wa mwaka 2017/2018.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.