Na Yuster Sengo
Mkuu wa wilaya ya Ulanga M Ngollo Malenya amemtaka kaimu mwenyekiti wa kijiji cha Iputi Bw.Fadhili Hassan kujiengua katika wazfa huo ifikapo tarehe 3 septemba mara baada ya kikao cha kusoma mapato na matumizi ya kijiji hicho
Hatua hiyo imekuja mara baada ya sintofahamu kuhusu uongozi wa kijiji hicho ambapo viongozi wa kijiji hicho wanakaimishana bila kufuata taratibu na miongozo inayotakiwa
Akizungumza katika kikao hicho ,Bw Twaha Athuman ambaye ni mkazi wa Iputi amesema kuwa halmashauri ya kijiji hicho imekuwa ikikaimishana uongozi kwa watu bila kushirikisha wananchi hali inayowapa wasiwasi wananchi
“kumekuw na tabia ya kukaimishana uongozi wenyewe kwa wenyewe bila kutupataarifa wananchi au hata kuitisha mkutano ili kuwatambulisha na wananchi kuridhia,sasa tangu mwenyekiti tuliemchagua yupo kizuizini lakini tangu awekwe kizuizini kumakuwa na makaimu karibia sita hali inayomyumbusha afisa mtendaji kuleta maendeleo”amesema Bw. Twaha
Akizungumzia sheria ya jinsi ya kukaimishana ofisi,Joseph Mkude ambaye alikuwa anamuwakirisha mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ulanga Bw. Yusuph Semguruka amesema kuwa kabla ya kukaimisha ofisi kwa mtu yeyote ni lazima wananchi waridhie na kumkubali anayekaimishwa nafasi hiyo
“hauwezi kumpa mtu uongozi kwa kuwa unamtaka wewe,utaratibu ni kuwa unaitisha mkutano wa kijiji na kuachia wananchi wapendekeze mtu wanaemtaka wakisha ridhia kwa pamoja ndio anapitishwa kushika uongozi huo
Hata hivyo mkuu wa wilaya amewasisitiza wakazi wa kijiji hicho kuhudhuria kikao kitakachoitishwa septemba 6 mwaka huu ili kusukiliza ripoti ya mapato na matumizi na baadaya hapo kumtaka makamu mwenye kiti wa kijiji anayekaimu kwa sasa kuachia nafasi hiyo ili kufata utaratibu uanaotakiwa
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.