Na
Fatuma Mtemangani
Mkuu wa wilaya ya Ulanga Bi. Ngollo Malenya amewataka wananchi wa Ulanga kushirikiana pamoja katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara kwani huduma hiyo ikikamilika itawanufaisha wananchi wote.
Mkuu wa wilaya ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika tarafa zote zilizopo wilayani Ulanga na kufanya mkutano hadhara ili kujua changamoto zinazowakabili wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Hata hivyo amewataka viongozi wa kata,vijiji na vitongoji kuitisha mikutano kwa lengo la kuhamasisha wanachi kutoingiza mambo ya siasa kwenye swala la maendeleo na badala yake wachangie shughuli za maendeleo kwa ajili ya vizazi vya sasa na baadae.
“Jamani shughuli za maendeleo hazina chama naombeni tumuunge mkono rais wetu wa jamhuri ya ,muungano wa tanzania Daktrari John Pombe Magufuli anafanya maendeleo bila kujali itikadi ya chama chochote,kabila wala rangi na ndiyo maana tunapata maendeleo mazuri na kwa wakati lakini angefuata mambo ya chama na ukabila leo hii tusingekuwa na maendeleo”.alisema Ngollo.
Pia Bi. Ngollo amewataka viongozi kushirikiana kwa pamoja ili kuijenga Ulanga mpya yenye mafanikio na kuacha maneno ambayo hayataifikisha ulanga mahali sahihi hivyo wanapaswa pia kuwashirikisha wananchi katika shughuli mbalambali za maendeleo ya vijiji kwa kufyatua matofali,kusomba mchanga,mawe katika kumalizia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari, na uchangiaji wa bima ya afya CHF iliyoboreshwa.
Aidha katika ziara hiyo mkuu wa wilaya ameongozana na viongozi mbalimbali wa halmashauri akiwemo katibu TAWLA wa wilaya ndugu Abraham Mwaikwira,mganga mkuu wa wilaya Daktari Rajabu Risasi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ili kuangalia juhudi zinazofanywa na wananchi.
Mkuu wa wilaya amefanya ziara katika tarafa ya ikiwemo tarafa ya Mwaya,Lupiro,ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake kwa kutembelea mgodi wa mdini wa Epanko na kutazama namna ya kuwasaidia wachimbaji wadogo ambao kidogo wanaonekana kuyumba kiuchumi.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.