Wakandarasi wanaokuja wilayani Ulanga kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali wahetakiwa kuzingatia sheria ya usalama kwa vibarua wao.
Hayo yamesemwa na Mh. Msalam Mohamed Msalam wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyofanywa na kamati ya Fedha, Utawala na Mipango hivi karibuni
Mh. Msalam alisema kuwa wakandarasi wengi wamekuwa hawazingatii usalama wa vibarua wanaowajiiri katika maeneo yao ya kazi hali ambayo inahatarisha usalama wao kwani wanaweza kuumia kirahisi sababu hawajapewa vifaa vya kuwakinga.
Aliongeza kuwa pamoja na kuwakinga vibarua na kuumia wakandarasi hao wanaenda kinyume na kanuni za bodi ya wakandarasi ambao wanasisitiza usalama wa vibarua kwanza na kutozingatia hilo ni kupuuza utekelezaji wa kanuni hizo.
Aidha alimwagiza mkandarasi anayetekeleza mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Mavimba kuwanunulia vifaa vya usalama vibarua wake ikiwamo mabuti na kofia ngumu ili kuwaweka katika hali ya usalama zaidi.
Ziara ya waheshimiwa madiwani wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango imefanyika kwa siku mbili kwa kutembelea miradi ya maendeleo ikiwa ni ziara ya robo ya nne na miradi mbalimbali ilitembelewa na kutolewa maoni na ushauri katika miradi hiyo ili itekelezwe kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.