Na Yuster Sengo
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga kwa mara ya kwanza imeadhimisha siku ya Mashujaa kwa kufanya Ibada/Dua na kuweka mashada ya maua kwenye kaburi lililozikwa Mashujaa zaidi ya 3000 waliopigana vita ya majimaji mwaka 1905-1907
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mh. Ngollo Malenya amesema kuwa Serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua umuhimu wa Mashujaa waliokufa kwenye vita na ndiyo maana imewekwa tarehe rasmi kwaajili ya kuenzi maadhimisho ya Mashujaa
“Tumekusanyika hapa kwakuwa tunatambua mchango wa Mashujaa waliopigana vita kwaajili ya kupigania Uhuru na Serikali pia inatambua mchango wa Mashujaa wetu ndiyo maana kukawa na Tarehe rasmi ya maadhimisho hayo”Amesema Mh. Ngollo
Hata hivyo akizungumza katika maadhimisho hayo Afisa Tawala bi. Huruka Rajab amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Ulanga na Ofisi ya Mkurugenzi kwa kufanya juhudi ya kukarabati eneo hilo la kaburi la Mashujaa na kulifanya liwe na hadhi inayotakiwa kwa kuweka mnara
“Hili eneo lilikuwepo lakini Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wamefanya juhudi ya kujenga Mnara huo kwaajili ya kumbukumbu ya Mashujaa waliopigana vita 1905-1907”Amesema Bi.Huruka
Naye Afisa Maliasili Bi. Florencia Massawe akisoma Taarifa ya Maadhimisho ya siku ya Mashujaa amesema kuwa siku hii huadhimishwa tarehe 25/7 kila mwaka na sababu ya maadhimisho haya ni kuenzi Mashujaa waliopigana vita mwaka 1905-1907 baada ya waafrika kulazimishwa kulima Pamba bila ujira
Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika katika eneo la kaburi la Mashujaa lililopo katika kijiji cha Chamange imeleta historia mpya kwani Maadhimisho hayo yamefanyika kwa mara ya kwanza wilayani Ulanga kwa kuzuru Eneo hilo na Kufanya Dua/Sala fupi kwaajili ya kuwaombea Mashujaa waliozikwa mahali hapo
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.