ULANGA
Na Fatuma Mtemangani
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilayani Ulanga Mkoani Morogoro ndugu Yusuf Daud Semuguruka amewataka wakazi wa kijiji cha vigoi kuwa na subira wakati serikali inatekeleza ujenzi wa miundo mbinu ya bara bara ili ipitike kwaurahisi hasa kwa kipindi hiki cha mvua za masika.
Akizungumzia changamoto ya miundo mbinu hiyo Mkurugenzi amesema kua tatizo la miundo mbinu ya barabara tayari ameifanyia kazi hivyo amewaomba wananchi kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki wakati serikali inafanya jitihada ya kutatua changamoto hiyo.
Hata hivyo ameongeza kua wananchi wanapata shida kupita katika barabara hizo kutokana na tope zilizo sababishwa na vifusi walivyo weka bila kusambazwa lakini kwa sasa tayari jitihada za kusambaza vifusi hivyo imeanza kufanywa na mkandarasi.
Ndugu Semuguruka amesema kua halmashauli imeanza kuweka vifusi katika barabara hizo hali itakayopelekea kupitika kwa urahisi kwa barabara hizo katika kipindi cha masika na kiangazi.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.