Ulanga
Na Fatuma Mtemangani
Zaidi ya shilingi milioni 300 zimetumika Katika mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF Wilayani Ulanga mkoani Morogoro kwa kipindi cha mwezi wa tatu hadi wanne kusaidia kaya zipatazo 4807 sawa na asilimia 99 ya kaya zote zilizopo katika mpango huo kwa mwaka 2017.
Akizungumza na Redio Ulanga Fm kaimu mratibu wa TASAF bi, Jackilin Mponguliana amesema pamoja na kuwapatia fedha hizo TASAF imesaidia kuwawezesha wanufaika juu ya elimu ya ujasiriamali ikiwemo ufugaji wa kuku na nguruwe ili kuwa na uhakikika wa kipato na kukidhi mahitaji yao ya msingi.
Aidha kwa upande wa wanufaika wa mpango huo wameieleza Ulanga Fm kuwa elimu ya ujasiriamali waliyoipata kupitia TASAF pamoja na uwezeshwaji wa fedha imewasaidia kuanzisha miradi midogo midogo kwa kutumia ruzuku wanazopata na kukidhi mahitaji yao ikiwemo uhakika wa chakula, pamoja na gharama za elimu kwa watoto wao.
Mpango wa kunusuru kaya masikini {TASAF}ulianzishwa mnamo oktoba 2014, kuwajenga uwezo kwa viongozi ngazi ya wilaya,kuunda na kufundisha timu ya wawezeshaji wa wilaya,utambuzi na uandikishaji wa kaya masikini katika vijiji 47 vilivyo katika mpango ambavyo ni sawa na 51% kati ya vijiji 29 vya wilaya ya Ulanga.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.