NA FATUMA MTEMANGANI
Mradi wa kupambana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kwa makundi maalumu na yaliyo katika hatari zaidi katika ngazi ya jamii ujulikanoa TANZANIA HEALTH PROMOTION SUPPORT (T H P S) umetambulishwa leo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro kwa lengo la kutoa Elimu kwa jamii juu ya mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI .
Katika kutambulisha mradi huo wadau mbalimbali walialikwa wakiwemo viongozi wa dini ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Ulanga bi.Ngollo Malenya lakini aliwakilishwa na mkurugenzi mtendaji ndugu Yusuph Semuguruka ambapo ameshukuru mradi huo katika mkoa wa Morogoro wilaya ya Ulanga ndiyo Wilaya ya kwanza kuanza kufanya kazi.
“Ndugu Semguruka alisema kuwa shirika pia liangalie mavazi wanayovaa watoto wa kike na pia kujitambua kwani hiyo huleta vishawishi kwa baadhi ya wanaume,na pia alitaka kujua kwa watoto ambao ni wasichana balehe wa shule za msingi ambao wanasahaulika sana na wanafunzi wa shule za sekondari wanaachwa na wazazi wao wakati wa kilimo wazazi wanahamia shamba na kuwaachia majukumu ya kifamilia je kama mradi mnawezaje kulidhibiti hilo?”Aliuliza Semuguruka.
Akijibu swali hilo mwezeshaji katika uzinduzi huo bi. Vaileth Moshiro alisema kuwa shirika litafanya jitihada ya kuwafikia makundi hayo na kutoa elimu juu ya maambukizi mapya ya VVU,kuunda vikundi kama vikoba pamoja na kuwapatia elimu ya ujasiriamali,kuwapatia mitaji,kuwahudumia kitabibu,kuwapatia madawa na vipimo pale vitakapohitajika pia kwa upande wa wazazi shirika litatoa elimu kwa wanafuzni hao na wazazi ili wazazi waondokane nah ii dhana ya kuacha watoto nyumbani peke yao wakati wa kilimo.
“wadau wetu watafanya kazi kwa karibu na T H P S na kwa uangalizi wa ofisi ya mganga mkuu wa mkoa na mganga mkuu wa wilaya kuhakikisha mradi unafikia malengo tuliyokusudia katika wilaya yetu ya Ulanga na watu watabadilika kwani Ulanga bila UKIMWI inawezekana”Alisema mkurugenzi.
Hata hivyo bi.Vaileth Moshiro ameongeza kuwa mradi huo umelenga makundi maalumu wakiwemo wanaotumia madawa ya kulevya,wasichana balehe na wanawake vijana,wafanyabiashara wakubwa,kambi za wavuvi,watu wenye ulemavu na wanaofanya biashara ya ngono(madanga)lengo kubwa ni kuwasaidia kiuchumikwa wabadilike kitabia kwa kupunguza maambukizi ya UKIMWI.
Pia bi Vaileth Moshiro amewaomba viongozi wa dini walihudhuria katika utambulisho wa mradi huo kuhubiria hali ya hatari ya maambukizi katika nyuma za ibada na kufikisha ujumbe huu kwa makundi maalumu katika wilaya ya Ulanga.
Aidha mkurugenzi amewapongeza na kuwashukuru mradi huo unaoendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI lakini pia vita dhidi ya VVU kwa kusaidiwa na Global Fund ambao unatoa elimu hii kwa mikoa mitano nchini Tanzania na kwa wilaya ya Ulanga utafanyakazi kwa miaka mitatu.
Ili kutokomeza kupunguza maambukizi ya VVU nchini kuweza kutokomeza UKIMWI duniani ifikapo mwaka 2030,ni dhahiri kuwa tunao wajibu wa kuweka mipango na mikakati ya kupambana na vvu na UKIMWI kwa makundi haya,kutokana na UKIMWI kwa makundi haya yapo juu sana kulinganisha wastani wa kiwango cha maambukizi nchi nzima.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.