Viongozi wilayani Ulanga wamepongezwa kwa kuibua na kuhamasisha miradi yenye manufaa kwa wananchi.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Tawala Msaidizi Bwana Noel Kazimoto katika ziara ya ukaguzi na uhamasishaji na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ndani ya wilaya akiwa na viongozi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Safari Road Afisa Mtendaji wa Kijiji Bi. Sophia Haule amesema kuwa ujenzi huo uliibuliwa na wananchi na viongozi kutokana na kukosekana kwa ofisi ya kijiji na kuwalazimu kupanga ofisi ambayo ni finyu na gharama.
Aidha aliongeza kuwa ujenzi umefanikiwa kutokana na msaada wa nguvu za wananchi, fedha za Halmashauri na fedha za mfuko wa jimbo ambapo hatua iliyofikia ni umaliziaji na uwekaji wa samani.
Akipokea taarifa hiyo Bwana Kazimoto aliwapongeza viongozi wa kijiji hicho na watu wote waliochangia ujenzi huo hadi hatua hiyo na kuwakumbusha kusoma mapato na matumizi ya ujenzi huo na kuwashauri kuendelea kubuni miradi yenye manufaa kwa wananchi.
Hata hivyo Bwana Kazimoto aliwataka wakuu wa Idara kusimamia miradi yote ndani ya wilaya na kufanya ufuatiliaji katika ngazi za chini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki na kwa wakati.
Ziara ya ufuatiliaji wa miradi imefanyika wilayani Ulanga na mkoa kwa ujumla ikihusisha viongozi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI na ofisi ya Katibu Tawala Mkoa ambapo kwa wilaya ya Ulanga walitembelea miradi ya ujenzi wa vyoo shule ya Msingi Mahenge Mjini, ujenzi wa soko la Kijiji cha Mahenge, maabara shule ya sekondari Mahenge na ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Safari Road..
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.