Na.Yuster Sengo
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Kange Lugola amelitaka jeshi la polisi wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro kuhakikisha kutokuwepo kwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji au wakulima kwa wakulima katika wilaya hiyo
Akizungumza katika mkutano na wananchi katika viwanja vya stand ya zamani , Waziri Lugola amesema kuwa jeshi la polisi lihakikishe hakuna migogoro ya mipaka itakayotokea na hata kama ikitokea wahakikishe hakutakuwa na mapigano , kuumizana wala vifo vitakavyotokana na migogoro hiyo
Aidha amewaonya polisi kutokutumika katika vitendo vya kudhurumu mali za watu au kutetea upande usiyo na haki au kudhurumu mali na kumpa asiyekua na haki
“polisi nisisikie mnatumika katika vitendo vya udhurumati,unakuta polisi anajua kabisa hii mali ni ya fulani lakini anatetea upande wa yule ambaye siyo mali yake na baadae anakabidhiwa hiyo mali kitendo ambacho si cha kiungwana kabisa ,tusimame kwenye ukweli na tulinde mali za raia”Amesema Lugola
katika hatua nyingine mh kangi lugola amewataka wananchi wilayani ulanga kuhakikisha wanatokomeza tatizo la ubakaji
mh kangi amewataka viongozi wa wilaya kuhakikisha wanachunguza chanzo cha tatizo la ubakaji kwani inawezekana wapo watu wanadanganywa na waganga ili kujipatia madini
“Hapa wilayani kuna migodi mingi ya madini mbalimbali ,sasa polisi mchunguze ni kwanini vitendo vya ubakaji vinaongezeka ,inawezekana labda ni masharti ya mganga,sasa mchunguze mjue ukweli wa suala hili”Ameongeza Mh Lugola
aidha mh wazrii amewataka polisi kuchunguza na kuwakamata wale wote wanaojihusisha makosa ya ubakaji kwani ni tatizo ambalo linawezekana kuzuilikia
waziri wa mambo ya ndani nchi amemaliza ziara yake wilayani ulanga kwa kusikiliza kero za wananchi waliojitokeza kumsikiliza
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.