• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Eneo la Utawala
    • Majukumu ya Viongozi
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi na Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Radio Ulanga FM
      • Ijue Radio Ulanga FM
      • Vipindi vya Radio Ulanga FM

Naibu Waziri wa Madini asitisha uchimbaji wa Madini kijiji cha Epanko Wilayani Ulanga

Imetumwa: July 12th, 2018

ULANGA

 

Na

Fatuma Mtemangani

 

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko amesimamisha shughuli za uchimbaji madini ya kinywe na vito katika machimbo ya Epanko yaliyopo katika wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro ili Serikali iweke kwanza utaratibu mzuri wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji madini katika eneo hilo kabla ya kuruhusu uchimbaji madini kuendelea.

Biteko alitoa agizo hilo tarehe 10 Julai, 2018 kwenye ziara yake aliyoifanya katika machimbo hayo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji madini pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Kamati iliyoundwa na Tume ya Madini kwa ajili ya kuchunguza shughuli za uchimbaji madini katika machimbo hayo.

Hivi karibuni, Naibu Waziri Biteko alielekeza Tume ya Madini kuunda kamati hiyo kwa ajili ya uchunguzi huo na kuwasilisha taarifa yenye mapendekezo ya namna ya kuboresha uchimbaji katika machimbo ya Epanko.

 Naibu Waziri Biteko mara baada ya kutembelea eneo hilo na kushuhudia shughuli za uchimbaji madini zikiendelea pasipo kufuata kanuni za mazingira huku katika baadhi ya maeneo mitambo ikiwa imefungwa kwa ajili ya kuondolewa, aliagiza wamiliki wa leseni kukusanya vifaa vya uchimbaji madini chini ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na kusimamisha shughuli za uchimbaji madini ndani ya siku tatu hadi Serikali itakapojiridhisha juu ya mwenendo wa shughuli za uchimbaji madini.

Aliendelea kusema kuwa, katika eneo hilo kumekuwepo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za mazingira kwa kuchepusha mto Kilombero hali iliyopelekea uharibifu mkubwa wa mazingira

Alisema kuwa wachimbaji madini wamekuwa wakitiririsha maji machafu kutoka migodini kwenda kwenye mto Kilombero ambao ni tegemeo kubwa la wananchi wanaozunguka eneo la Epanko jambo ambalo linahatarisha afya zao.

Alisisitiza kuwa wachimbaji madini wengi wamekuwa wakiendesha shughuli zao pasipo kuwa na vibali vya mazingira kama sheria na kanuni za uchimbaji madini zinavyowataka.

Aliongeza kuwa kumekuwepo na changamoto ya kutokuwepo kwa uwazi katika mikataba kati ya wamiliki wa leseni na kampuni zinazoendesha shughuli za uchimbaji madini, mapato na kodi mbalimbali zinazotakiwa kulipwa serikalini.

Kumekuwepo na malalamiko kwa baadhi ya wamiliki wenye leseni kudhulumiwa haki zao na kampuni zinazoendesha shughuli za uchimbaji madini na kusisitiza kuwa ni vyema Serikali ikasitisha shughuli zote za uchimbaji madini katika eneo la Epanko na kuanza ukaguzi wa leseni moja moja ili kuona kama zinakidhi sheria na kanuni za madini kabla ya kuruhusu shughuli za uchimbaji madini kuendelea.

Katika hatua nyingine, Biteko alielekeza uanzishwaji wa Ofisi ya Madini katika wilaya ya Ulanga itakayosimamia kwa karibu mwenendo wa shughuli za uchimbaji madini katika wilaya hiyo.

Awali akitoa taarifa ya kamati iliyoundwa kwa ajili ya uchunguzi wa shughuli za uchimbaji madini ya kinywe na vito katika machimbo ya Epanko, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Prof. Shukran Manya alisema kuwa kamati hiyo ilibaini kuwa uchimbaji madini katika eneo hilo ulikuwa hauzingatii sheria na kanuni za madini pamoja na mazingira na kutokuwepo kwa uwazi katika mapato na matumizi katika migodi.

Aliongeza kuwa kamati ilibaini kutokuwepo kwa mikataba kati ya wamiliki wa leseni za madini na kampuni zinazoendesha shughuli za uchimbaji madini zilizosajiliwa kwenye Ofisi za Madini na Halmashauri hali ambayo imekuwa ikisababisha migogoro ya mara kwa mara.

Alitaja wachimbaji wanaofanya kazi katika eneo la Epanko kuwa ni pamoja na Peter Chamtitu, Jonas Mpanduli, Sabinus Chigumbi, Franone & Gems na Paskali Jonas Mpanduli & Partners ambao wamelipa mrabaha hadi sasa.

Alitaja wachimbaji wengine ambao hawajalipa mrabaha mpaka sasa kuwa ni pamoja na Mathias Osward Lunkombe & Partners, John Joseph Ntoga na Protas Osward Lunkombe, Moshi Saidi Nassoro na Christoms Martin Msakamba na Bonifas Julai.

Wachimbaji wengine ambao hawajalipa mrabaha ni Joseph Kabu Mworia, John Joseph Ntoga na Franone Mining & Gems Co. Ltd, Joseph Paulo Mwangu & Partners, Mohamedi Said Magonga & Partners, Interstate Mining Limited na Flora Amadei Lyaupe & Partners.

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA October 04, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI November 22, 2021
  • KUITWA KWENYE MAFUNZO YA MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI TARAFA YA VIGOI March 14, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022 May 06, 2022
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • Hakimu mfawidhi Ulanga atambulisha wiki ya sheria

    January 17, 2024
  • Hakimu mfawidhi Ulanga atambulisha wiki ya sheria

    January 17, 2024
  • Bonanza la Uhuru lafana Ulanga

    December 08, 2023
  • Kuelekea Siku ya 9 December Viongozi na Wananchi wa Wilaya ya Ulanga wafanya usafi katika Hospital ya Wilaya

    December 06, 2023
  • Angalia Zaidi

Video

Link Kuripoti shuleni
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Vipindi vya Radio Ulanga
  • Majukumu ya Viongozi wa Serikali za Mitaa
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA FFARS
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

    Anwani ya Posta: P.O. BOX 22

    Telephone: +2550232626340

    Simu: 0763845957

    Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.