Na.Yuster Sengo
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga Mh. Nassoro Kihiyo amewataka viongozi wa kata ya ruaha kuwaelimisha wananchi wa ruaha kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa corona na kufata yale yote yanayoagizwa na wizara ya Afya na Serikali juu ya kujinga na ugonjwa wa corona
Akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua mradi wa ujenzi wa soko la Ruaha , Mh.Nassoro amesema kuwa kwakuwa mtendaji ni kioo kwa wananchi basi ajitahidi kuonesha mfano kwa wananchi kwa kuvaa barakoa ili wananchi hao waige kutoka kwake
“tuchukue tahadhari , watu wengine wana huu nugonjwa lakini hawaoneshi dalili zozote , Mtendaji wewe ni kioo kwenye hukchi kijiji , na wewe mwenyekiti wa kijiji na wewe pia ni kioo kwenye hichi kijiji cha Ruaha, tunategemea tukija hapa tena tukute umechukua tahadhari ili wananchiwengine wapate mfano kutoka kwako”Amesema Mh Kihiyo
“Na barakoa hizi siyo lazima za kununua za elfu tatu moja,,ukichukua tu kitambaa ukashona ukaweka na mipira basi inafaa, hata kama huna kitambaa ukikata tu kanga unaweka layer mbili tu inafaa, kwahiyo ndugu zangu tuchukue tahadhari”Ameongeza Mh. Kihiyo
Wakati huo huo Mh.Nassoro ameipongeza kamati ya ujenzi ya soko hilo kwa kazi nzuri wanayofanya katika kuendeleza ujenzi wa soko hilo na kuwaahidi kuwa kamati ya fedha na mipango ya halmashauri itatafuta pesa kwaajili ya kujenga choo cha soko hilo ili mradi huo uanze kuwahudumia wananchi
Hata hivyo ameongeza kuwa hata kama suala hilo litashindikana kwa mwaka wa fedha huu ila halmashauri itajitahidi hata kwenye mwaka wa fedh ujao pesa itapelekwa ili kukamilisha choo na soko kuanza kufanya kazi
“haya mambo ya fedha ni mambo ya kawaida katika mradi wowote, mimi sijawahi kwenda kwenye mradi wowote ambao hauna shida ya hela , mimi najua mtatafuta jinsi na mtapata fedha hizo kidogo zilizo pelea za kumalizia , kwasababu kama misumali kilo tano imebakia mi nadhani mtafanikiwa tu”Amesema Mh.Kihiyo
mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.