NA YUSTER SENGO
HATIMAE MWENGE WA UHURU UMEPOKEWA KATIKA WILATA YA ULANGA UKITOKEA WILAYA YA MALINYI BAADA YA KUKIMBIZWA KWA SIKU SITA KATIKA WILAYA MBALI MBALI ZA MKOA WA MOROGORO
AMBAPO KATIKA WILAYA YA ULANGA UMEKIMBIZWA KWA KILOMITA 230 HUKU ZAIDI YA MIRADI TISA YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1966 IMETEMBELEWA NA MWENGE HUO WA UHURU
AIDHA MCHANGANUO WA MIRADI HIYO NI PAMOJA NA MILIONI 147 IMETOKA SERIKALI KUU,MILLIONI 25 IMETOKA HALMASHAURI ,MILIONI 142 MICHANGO YA WANANNCHI NA BILIONI 1.651 KUTOKA KWA WADAU WA MAENDELEO
AIDHA MIRADI ILIYOWEKEWA JIWE LA MSINGI NA MBIO ZA MWENGE NI MITANO IKIWA NI PAMOJA NA UJENZI WA MADARASA MAWILI YA SHULE YA MSINGI NAKAFULU,OFISI YA WATUMIAJI MAJI LUPIRO,MRADI WA KARANGA MITI NA SOKO LA MAZAO MAHENGE
MIRADI MINGINE ILIYOPITIWA NI PAMOJA NA MRADI WA NG’OMBE ,UFUGAJI WA KUKU NALUKOO,MRADI WA THAMANI YA MAZAO LUPIRO
HATA HIVYO KATIKA ENEO LA MKESHA ULIOFANYIKA TARAFA YA MWAYA ,UPIMAJI WA AFYA ULIFANYIKA AMBAPO UPIMAJI HUO ULIJUMUISHA UPIMAJI WA UGONJWA WA UKUMWI,UPIMAJI WA UZAZI WA MPANGO ,PAMOJA NA UPIMAJI WA SARATANI WA MLANGO WA KIZAZI
AIDHA TAKWIMU ZILIZOTOLEWA BAADA YA UPIMAJI HUO,KATIKA UPIMAJI WA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI,WATU WALIOJITOKEZA KUPIMA NI ASILIMIA 51 AMBAPO WANAWAKE WALIOJITOKEZA NI ASILIMIA 45 NA WANAUME NI ASILIMIA 55 AMBAPO WALIOGUNDULIKA NA MAAMBUKIZI NI SABA ,KATI YA HAO SABA WANAWKE WALIOKUTWA NA MAAMBUKIZI NI 3 NA WANAUME NI 4 SAWA NA ASILIMIA 1.34
KATIKA UPIMAJI WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI WANAWAKE 200 WALIJITOKEZA KUPIMA ,WANAWAKE 8 AMEKUTWA NA MAAMBUKIZI YA UGONJWA HUO
MWENGE WA UHURU ULIKABIDHIWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOMBERO SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 28/7/2017 UKITOKEA WILAYA YA ULANGA
KAULI MBIU YA MWENGE WA UHURU MWAKA HUU NI ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA WEKEZA SASA KWA MAENDELEO YA TAIFA
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.