Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Bwana Yusuf Semuguruka amewata walimu wote waliopewa dhamana ya kusimamia mitihani ya darasa la saba kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa.
Akizungumza ofisini kwake Bwana Semuguruka alisema kuwa serikali imetumia gharama kubwa kuwapatia semina elekezi wasimamizi wote wa mitihani na hivyo hatarajii kusikia vitendo vya udanganyifu vikitokea.
Aidha Bwana Semuguruka alwataka wazazi wa wanafunzi watakaofanya mitihani kuhakikisha wanawajengea mazingira rafiki watoto wao ili kuwaondolea hofu ya mitihani na hatimaye wakafanya vizuri.
Pamoja na hilo aliwahakikishia wanafunzi wanaomaliza masomo yao ya darasa la saba kuwa halmashauri imewaandalia mazingira mazuri kwa shule za sekondari watakazo chaguliwa kujiunga ikiwa ni pamoja na uwepo wa madawati ya kutosha na miundombinu ya kujifunzia.
Mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi nchini unafanyika tarehe 6 na 7 septemba mwaka huu ambapo kwa wilaya ya Ulanga jumla ya watahiniwa 2667 wamesajiliwa kufanya mtihani huo ambapo kati ya hao watahiniwa 10 ni wenye uono hafifu ambao watapewa mtihani wa maandishi makubwa.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.