ULANGA
NA
Fatuma Mtemangani
Halmashauri wilaya ya Ulanga ni kati ya Halmashauri 9 zinazotekeleza Mradi wa Tusome Pamoja kwa Mkoa wa Morogoro na lengo la mradi huo ni kuimarisha Stadi za ujifunzaji na kujenga umahiri katika kusoma , kuandika na kuhesabu, kwa wanafunzi wa madarasa ya chini hususani kwa darasa la kwanza na darasa la pili.
Akizungumzia kuhusu mradi huo Afisa Elimu msingi Bi.Rehema Nyoka alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuhamasisha na kuelimisha ili kuleta maendeleo mazuri ya mtoto ikiwemo utunzaji wa vitabu kwa kuwa na vituo vya utunzaji kwa kujengewa uwezo wa uhamasishaji wa jamii katika kumuwezesha mtoto kujifunza akiwa shuleni.
Bi Nyoka aliongeza kuwa pia kuwaangali watoto wapi walipojifunza na wamejua kusoma,kuhesabu na kuandika yaani [KKK] kwa kuangalia aina ya kujifunza kwa kurudia,kinga,kukosea,kujaribu na kutenda.
Mradi wa Tusome Pamoja umeleta mabadiliko makubwa katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali hivyo hali ya Miundombinu , Ujenzi wa madarasa unaofanywa na jamii, kwa upande wa nguvu kazi ya jamii,na uchangiaji wa fedha taslimu unatekelezwa kwa wakati hali iliyopelekewilaya ya Ulanga kufanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba na mpaka sasa hakuna mwanafunzi yeyote anayefanya mtihani wa darasa la IV na la VII wasiojua Kusoma,Kuhesabu na Kuandika,hapi inayopelekea wilaya ya Ulanga kuendelea kufanya vizuri katika Shule za Msingi.
Aidha, kupitia uhamasishaji wa Elimu kwa jamii,imepelekea Elimu Jamii kuhamasika kuchangia chakula, kwa shule 42 sawa na 68.8 % zinatoa chakula cha mchana hivyo kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi 2018 na kupelekea wanafunzi waliomaliza darasa la nne na la saba wanajua kusoma,kuhesabu,na kuandika.
Hata hivyo Suala la utoaji wa lishe shuleni limesaidia kwa kiasi kikubwa na kupelekea kuimarisha stadi za Kusoma na kuandika,uhamasishaji wa jamii, ushiriki hai wa wazazi na jamii katika kusimamia Elimu hususani Miradi ya Maendeleo , ufuatiliaji na uthibiti wa utoro shuleni, na utoaji wa lishe.
Pia kulikuwa na changamoto mbalimbali walizokumbana nazo,na hatua ambazo zilichukuliwa katika baadhi ya shule na mafanikio yaliyopatikana hasa kwa upande wa miundombinu ya ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa, ufundishaji na ujifunzaji wa stadi za kusoma,kuandika na utoaji wa lishe shuleni .
Shukrani za peke kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wake Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kuukubali mradi huu wa Tusome Pamoja kwani umesaidia Kuimarisha Stadi za Ufundishaji wa Kusoma,Kuhesabu na Kuandika,kuimarika kwa ujuzi, mifumo ya utoaji taarifa na tathmini (Uongozi na Usimamizi),Ushiriki hai wa Wazazi na Jamii katika Elimu kusimamia miradi ya maendeleo, utoaji wa lishe na usimamizi wa mahudhurio ya lazima shuleni.
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga ina jumla ya Shule za Msingi 61 zikiwemo 60 za Serikali na moja Binafsi,pia Halmashauri ina jumla ya walimu 659 wakiwemo Wanaume 366 na Wanawake 293,Maafisa Elimu Kata 21 wanaume 19 na wanawake 2
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.