Na.Yuster Sengo
Mkuu wa wilaya ya ulanga hm, ngolo malenya amewataka wenyeviti na watendaji wa vijiji kusoma taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi wao na kukabidhin taarifa sahii za utendaji wao
Akizungumza katika baraza la madiwani mh, malenya amesema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi hao wa vijiji kutokuwa waaminifu kwa kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi wao sambamba na kukiuka taratibu za ukabidhi wa ofisi ambapo ametoa onyo kwa watakao kiuka watachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Niseme tu kwa watendaji watakao kiuka agizo hili watachukuliwa hatua za kisheria kwani kuna baadhi ya watendaji hawasomi kabisa taarifa ya mapato na matumizi na wala wanapoyoka nje ya kituo hawakaimishi ofisi hali inayoleta usumbufu kwa wananchi”amesema mh .Malenya
Aidha amesema kuwa ni vizuri viongozi kuunga mkono jitihada za mh, raisi wa jamuhuri ya muungano wa tanzania katika kuleta maendeleo ya nchi kwa kufanya uadilifu kwa kuchagua viongozi wenye sifa kwa masrahi ya vijiji na taifa letu kwa ujumla.
“Tumuunge mkono rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania dk john pombe magufuli na juhudi anazo fanya kwa kujenga taifa letu kwa kuchagua viongozi wenye sifa na uadilifu”ameongeza mh . Malenya
Wilaya ya ulanga ni miongoni mwa wilaya iliyopo mkoani morogoro ambapo inajumla ya vijiji 59 vinavyotarajia kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika novembar mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.