Na Yuster Sengo
MKUU WA WILAYA YA ULANGA MH NGOLO MALENYA AMEWATAKA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA ULANGA KUWAELEKEZA WANANCHI WANAOVAMIA MAENEO YA HIFADHI KUACHA KUFANYA HIVYO MPAKA MAELEKEZO YA SERIKALI YATAKAPOTOLEWA JUU YA MATUMIZI YA SEHEMU YA HIFADHI
KAULI HIYO IMETOLEWA LEO KATIKA KIKAO CHA BARAZA MAALUM LA MADIWANI KILICHOFANYIKA UKUMBI WA PAULINE KWA AJILI YA KUJADILI BAJETI YA FEDHA YA MWAKA 2019/2010 AMBAPO MADIWANI WAMEJADILI NA KUPISHA BAJETI HIYO
AIDHA MKUU WA WILAYA AMEWASISITIZA MADIWANI KUWAASA WANANCHI KUACHA KUFANYA SHUGHULI ZA KILIMO NA UFUGAJI KATIKA MAENEO YA VIJIJI NA VITONGOJI VILIVYO KATIKA MAENEO YA HIFADHI LIYOTENGWA NA KUONGEZA KUWA KAMA KUNA DIWANI YEYOTE ATABAINIKA KUHAMASISHA WANANCHI KUFANYA SHUGHULI KATIKA MAENEO HAYO ,HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE
“TUSIWAHAMASISHE WANANNCHI KWENDA KUVAMIA MAENEO HAYO ,BADALA YAKE TUSUBIRI MAELEKEZO YA SERKALI KUHUSU SUALA HILO”AMEONGEZA MH .MALENYA
MKUU WA WILAYA AMESEMA KUWA WANAULANGA WANAWAAMINI WAO KAMA VIONGOZI WAO HIVYO HAWATAKIWI KUTUMIA NAFASI HIYO KUNUNJA SHERIA NA KUHARIBU UTARATIBU WA MATUMIZI YA HIFADHI KWA MAKUSUDI KAMA AMBAVYO BAADHI YA WANANCHI WALIANZA KUVAMIA MAENEO YA HIFADHI
AIDHA MH NGOLO AMESEMA KUWA WAPO MADIWANI WANAOHAMASISHA WANANCHI KUFANYA SHUGHULI KWENYE MAENEO YA HIFADHI HIVYO AMESEAMA KUANZIA SASA KIONGOZI YOYOTE ANAHAMASISHA WATU KUFANYA SHUGHULI KWNYE MAENEO YA YA HIFADHI HATU AKILI YA KISHERIA ITACHUKULIWA DHIDI YAKE.
“ITAKAPOBAINIKA KUWA KUNA KIONGOZI YOYOTE ANAWAHAMASISHA WANANCHI KUVAMIA MAENEO YALIYOTENGWA KWAAJILI YA HIFADHI,BASI HATUTASITA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHRIA VIONGOZI HAO”AMESEMA MH MALENYA
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.