Ulanga
Na
Fatuma Mtemangani
“Inashangaza sana kuona bado mnazikumbatia mila na desturi kandamizi zinazo wanyanyasa Wanawake,kwani Wanawake pia wanayo nafasi na haki ya kupanga na kuamua mambo hivyo tuache kuwaamulia vitu wasivyovitaka”Alisema Malenya.
Mh.Ngollo Malenye ameyasema hayo wakati alipotembelea katika kijiji cha Mbuyuni kuzungumza na wafugaji waliovamia meneo yaliyotengwa kwa ajili ya malisho hivyo alipofika kijiji cha Mavimba aliwakuta vijana wa kiume kabila la wasukuma wakimlazimisha kuoa kwa nguvu mwanamke yaani [chagulaga].
Mkuu wa Wilaya amewataja vinara hao wa kujipatia wake kwa nguvu kupitia mila potofu[chagulaga] ni watatu akiwemo Ngalula Lukaba,Masanja Scania na Majiga Lutamuno na kusema kua watuhumiwa hao wametiwa mbaroni na watafikishwa mahakamani na huu ni mwendelezo wa maadhimisho ya kupiga ukatili kwa Wanawake.
“Nasema hivi hatuwezi kuwafumbia macho watua ambao bado wanaendeleza mila na tamaduni ambazo hazina faida yeyote kwa jamii sio wa kuwachekea chekea nataka wote wakamatwe na kesi zao ziende mahakamani haraka ili tabia hii iweze kukoma na iwe fundisho kwa wafugaji wengine kwa Wilaya ya Ulanga”.Alisema Malenya.
Hata hivyo mh.Malenye alisema kua zoezi la kuwakamata wahusika bado linaendelea na yeyote atakaebainika hatua kali zitachukuliwa kwani kitendo hicho kinatambulika kama ubakaji kwani vitendo hivyo wamekuwa wakifanyiwa mabinti wenye umri mdogo sana.
Aidha amewataka jamii ya wafugaji wote Wilaya ya Ulanga kuacha mila na desturi ya kuwalazimisha watoto wa kike kuolewa wakiwa na umri mdogo na badala yake wapeleke watoto shule wakapate elimu ili waweze kutimiza ndoto zao.
Mkuu wa Wilaya amewaonya watu wenye mila potofu Wilayani hapa na kusisitiza kuwa hilo halikubaliki kisheria na yeyote atakaebainika anaendelea na zoezi hilo hatosita kumchukulia hatua dhidi yake hivyo wanapaswa kufuata sheria na taratibu kwa kutenda haki kwa watoto wa kike.
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.