Na. Yuster Sengo
Mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh.Ngollo Malenya amempongeza hakimu wa mahakama ya wilaya ya Ulanga Mh. James Muhanusi Kwa adhabu ya kifungo cha maisha aliyoitoa kwa bw. Mohamed Ramadhani mwenye umri wa miaka 40 ambaye alikua anashtakiwa kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka saba
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika leo tarehe 26 february Mh Malenya amesema kuwa tabia hii ya ulawati na ubakaji kwa watoto umeanza kunyemelea katika wilaya hii hivyo wazazi na walezi wawe na tahadhari hiyo na huongeza kuwa yeyote atakaye fanya vitendo hivyo atapewa adhabu kali
“nalisema hili kwa masikitiko sana, kwakweli nikiwa kama mzazi ninasikitika sana,vitendo vya kulawiti watoto wetu vimeanza kukuwa sana hapa wilayani kwetu,nawaomba sana tuwe karibu na watoto ili waweze kutwambia yale yanayowasibu huko mitaani’’Amesema mh. Ngollo Malenya
“Watoto wengine wanakuwa hawawezi kusema wanayofanyiwa hadi pale wanapoonza kuathirika kiafya hivyo naomba tuwe nao karibu sana na kila mzazi pamoja na walimu tutuoe macho kila pande ili kuhakikisha haya madhara hayakui zaidina tuweze kuyatokomeza zaidi ”Ameongeza Malenya
Aidha amewataka afisa elimu sekondari na afisa elimu msingi kutambua kuwa watoto wanapokuwa shuleni ni dhamana yao na wanapokuwa nyumbani ni dhamana ya mzazi au mlezi hivyo ni aibu kusikia vitendo vya ulawati na ubakaji vinatokea mashuleni na kuongeza kuwa sheria itachukua mkondo wake
“kwa mfano huyo aliyefungwa maisha na wengine wapo mbioni naamini Mh. Hakimu atafanya haki kwa kila mmoja “Amesema Mh.Malenya
Akizungumza kwa niaba ya madiwani Diwani wa viti maalum tarafa ya Ruaha Mh. Elizabeth Mtunga amesema kuwa wamesikia kwa makini kile ambacho mkuu wa wilaya amekisema kuhusu ulawiti na ubakaji kwa watoto na kuahidi kulifanyia kazi suala hilo ili kuweza kupunguza na hatimae kuondoa kabisa vitendo hivyo katika wilaya ya Ulanga
“Mh. mkuu wa wilaya ,sisi kama madiwani tunaahidi kulisimamia suala hili la kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa watoto ili watoto wetu wawe salama na kuishi kwa amani
Mwisho

Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.