Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mh.Ngollo Malenya amepiga marufuku tabia ya baadhi ya vijana kuwalizimisha wanawake kufanya nao mapenzi kwa nguvu na kutaka kuwaoa bila ridhaa yao
Kauli hiyo imekuja baada ya wanawake kutoa malalamiko yao kwa mkuu wa Wilaya katika muendelezo wa ziara yake ya kupokea kero kwa wananchi wa vijiji vya Ulanga .
“ Kuna baadhi ya wanaume wanatabia ambazo hazifai kwenye jamii kwani wanalazimisha wanawake kufanya mapenzi bila wao kuridhia na pia wanawavizia wanawake wakiwa wanaenda shamba au kwenye mnada”Amesema Mh.Ngollo
“Kwa kitendo hicho mnachofanya ni ubakaji kama walivyo wabakaji wengine na hivyo serikali haitafumbia macho mtu au kikundi chochote cha watu wenye tabia hiyo ambayo inafaamika kwa jina la Chagulaga”Ameongeza Mh. Ngollo
Hadija Miraji Matana ni mkazi wa kijiji hicho cha Igumbiro ameiomba serikali ifatilie kwa ukaribu sana suala hilo la chagulaga kwani imekuwa ni kero kubwa na linawanyima raha wanawake wa kijiji hicho
“kuna baadhi ya vijana wanakuvamia kwa nguvu kutaka kufanya mapenzi na wewe,kama ukikataa wanakupiga viboko na hata baba yako au bwana wako anakuja kukugombelezea na yeye wanampiga viboko,kwahiyo hii imekua changamoto,usumbufu na kero”Amesema Bi.Hadija
James Renatus ni kijana kutoka katika kijiji cha Igumbiro ambaye hapa anaelezea maana ya kitendo hicho cha chagulaga
“Ni kama mnakuwa vijana kwenye kundi mnaenda kutembelea sehemu halafumkakutana na wanawake aidha mmoja au watatu ,mnawazunguka kwa kuweka duara na mnawalazimisha kati yenu achague mwanaume mmoja aliyempenda akikataa mnamkamata mnaingia nae vichakani na kumlazimisha kufanya mapenzi hi indo maana halisi ya neon chagulaga kutoka katika kabila la kisukuma “Amesema Bw. James
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.