Ulanga
Na
Fatuma Mtemangani
Mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Bi. Ngollo Malenya amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Malaika anaejenga banio katika kijiji cha Minepa kata ya Minepa kumalizia ujenzi huo ifikapo tarehe 17/12/2018 na asipotekeleza hilo sheria inafuata mkondo wake.
Bi.Ngollo ameyasema hayo wakati alipotembelea miradi mbalimbali ya Halmashauri kujionea utekelezaji wake na kuwataka wakandarasi kumalizia ujenzi kwa wakati ili kuwahi mvua za masika kwani inaweza kuharibu miuondo mbinu hiyo.
Hata hivyo mkuu wa wilaya amewataka mkandarasi anaejenga banio hilo kujenga kwa kiwango kizuri ili iweze kuwasaidia wananchi wa kata ya Minepa kujikwamua kiuchumi kwa kuzimudu familia zao,kwani sera ya Tanzania ya Viwanda pia inategemea kilimo hasa kulima kilimo biashara,kilimo cha kisasa na chenye tija.
“Natoa siku ishirini na moja nataka tarehe 17/12 mwaka huu kama mlivyoahidi kumaliza,nataka ujenzi huo ukabidhiwe rasmi kwa mkurugenzi kwani kalenda imezidi sana sasa nitafanya maamuzi magumu sana kama mradi huo hautamalizika kwa muda uliopangwa kwani tunataka kuwahi hizo mvua zisije zikaharibu miundombinu hii na wananchi wameusubiri mradi huo kwa muda mrefu sana”Alisema Ngollo.
Aidha ujenzi huo umefanyika kwa kujenga upya banio hilo kutokana na mkandarasi aliyeanza ujenzi kupata matatizo ya kiafya na kwa sasa mradi huo unatarajia kukamilika kwa kujengwa na mkandarasi wa kampuni ya Malaika na unatarajia kukamilika tarehe 17/12/2018 kwa maelezo ya mkandarasi anaemalizia ujenzi
Pia ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni mia sita na hamsini na sita mpaka kukamilika kwake hivyo wakazi wa Minepa wamefurahia kupata mradi huo kwani utawaongezea uzalishaji kwa kulima kilimo cha kisasa kwa msimu wa miaka miwili kwani hakuna changamoto ya soko hivyo utasaidia kwa wakulima wa Minepa na maeneo yanayozunguka mradi huo.
“Ndugu zangu wakazi wa Minepa mmepata bahati kubwa sana ya kupata mradi mkubwa kwa ajili ya kupata huduma hii muhimu ya kilimo hivyo nataka muutunze ili huduma ziendelee na tuweze kumuunga mkono mh.Rais wetu wa Jamhuri ya Muungango Dk.John Pombe Magufuli kwa Tanzania ya viwanda katika sekta ya kilimo na ukikamili mimi nitakuja kukagua nikiona hakuna utunzaji basi fursa zingine zikitokea hatutazileta hapa Minepa.”Ngollo Malenya.”
Lengo la Ujenzi wa mradi wa umwagiliaji Minepa ni kuongeza uchumi,kwa wakulima wadogo wadogo katika sekta kilimo na kufika uchumi wa kati wa viwanda ifikapo mwaka 2025 na umegharimu jumla ya shilingi milioni mia sita hamsini na sita.
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.