Na Yuster sengo
Mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh Ngollo Malenya ameweka adhma ya kutembelea vijiji vyote 59 vya wilaya hii lengo kuu likiwa ni kujitambulisha kwa wakazi wa vijiji hivyo pamoja kuhamasisha maendeleo
Akizungumza katika mkutano wa wananchi katika kijiji cha Mbuga mh Malenya amesema kuwa kwa kufika katika kijiji hicho zitaibuka changamoto mbali mbali hivyo atajitahidi kuwajibika kikamilifu kwa kuweza kutafuta suluhisho la chanagamoto hizo
Akizungumzia mikakati yake na wapi atakapo elekezea nguvu zake mkuu wa wilaya amesema kuwa,ataelekezea nguvu katika bank tofali,mimba za mashuleni ,uchomaji misitu hovyo , pamoja shughuli za kijamii
Aidha katika suala la bank tofali katika kijiji cha mbuga ilibainika kuwa hakukuwa na tofali hata moja sababu kubwa ikiwa ni wakazi wa kijiji hicho wamegomea kushiriki katika zoezi la bank tofali kwakua uongozi wa kujiji hicho kutokusoma ripoti ya mapato na matumizi kwa kipindi cha mwaka mmoja hivyo wananchi hao wamekosa haki ya kujua michango yao inaenda wapo na inafanya kazi gani
“wananchi najua katika suala la bank tofali na suala la mapato na matumizi najua mtakua na mengi ya kusema na mimi nitawapa nafasi muweze kutoa kero zenu kwasababu haiwezekani mtoe michango yenu halafu msijue matumizi yake katika maendeleo “amesema mkuu wa wilaya Mh Ngollo Malenya
Aidha amewataka wakzi hao wa Mbuga kujiunga na Bima ya afya kwakua ugonjwa haupigi hodi na marfa nyingine hali ya ugonjwa inaweza kukuta kipindi ukiwa hauna hata akiba kidogo hivyo ukiwa na bima ya afya inaweza saidia kipindi chote cha ugonjwa
Mh Ngollo amezungumzia suala la mimba za mashuleni na kusema kuwa ofisi yake itwachukulia hatua vijana wote wanaowapa mimba watoto wa shule na hata wale wanaojihusisha na mapenzi na wanafunzi na hata wazazi na walezi wanaoshirikiana katika kuwaficha wahusika wa mimba hizo na kumalizia masuala haya nyumbani
”tukimkamata mzazi au kijana anayeishi na mwanafunzi atakua mfano na atahadithia “amesema Ngollo
Hata hivyo amesisitiza wakazi hao kuacha tabia ya kuchoma misitu kwani ofisi yake haitalifumbia macho suala hilo hivyo kuwataka wakazi hao kushirikiana kutoa taarifa pale wanapo baini kuna mtu kachoma moto
“kwa suala hili tutachukua hatua stahiki ,tutahakikisha mnatajana kwa maana haiwezekani mtu achome msitu halafu asifahamike kwahiyo nitoe tu rai wananchi wote mtii sheria bila shuruti uchomaji wa misitu ni kosa na lazima tutunze misitu yetu kwaajili ya vizazi vya badae
Ziara hii ya Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mh Ngollo Malenya bado inaendelea katika vijiji vingine ambapo siku ya tarehe 3/9/2018 atakua katika kata ya Sali kuendelea na ziara ya kujitambulisha na kuhamasisha maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.