Na. Yuster Sengo
Mkuu wa wilaya ya ulanga mh, Ngolo Malenya ametangaza punguzo la asilimia 50 ya bei za nauli ya mahenge mpaka ifakara kufuatia gharama iliyopangwa na latra
Mh Malenya amesema hayo kufuatia sinto fahamu ya usafiri iliyotokea baada ya tangazo la kushuka kwa gharama za usafirishaji lililopokelewa tofauti na madereva pamoja na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji maarufu kama noah wilayani ulanga
Akisisitiza utiifu wa tamko hilo Malenya amesema kuwa nauli ni shilingi elfu tano kutoka mahenge kuelekea ifakara na dereva atakayekiuka maelekezo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufutiwa leseni
“Kwanzia muda huu ninao ongea na nyinyi hapa ,nauli kutoka mahenge hadi ifakara ni shilingi elfu tano na yeyote asiyekubaliana na gharama hizo apaki gari yake nyumbani au abebe harusi hapa hapa mahenge na siyo kutoka nje ya mahenge,na yeyote atakaye toza nauli juu ya elfu tano atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni yake “amesema Mh. Ngollo
Aidha bi malenya amewaonya madereva na wamiliki kuacha kupandisha gharama za usafiri kinyume na utaratibu uliopangwa na mamlaka husika
“Nawaoba sana madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri muache tabia ya kupandisha gharama za usafiri kiholela na kinyume na utaratibu uliopangwa na mamlaka husiaka” ameongeza mh.ngollo
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.