Na Yuster Sengo
Mkurugenzi mtendaji wa halmshauri ya wilaya ya Ulanga Ndg .Jonas Mallosa ametoa agizo kwa maafisa tarafa na maafisa watendaji kuwa ifikapo tarehe 1/5/2019 shule zote za kutwa ambazo zilikua hazitoi chakula kwa wanafunzi ,zianze kutoa chakula
Akizungumza katika kikao kazi cha maafisa tarafa,maafisa watendaji na wakuu wa idara, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo amesema kuwa utoaji wa chakula mashuleni ni muhimu kwani inasaidia kuongeza ufaulu na ni kwa faida ya watoto wetu
Aidha amewaagiza maafisa tarafa na watendaji wakafanye vikoa mapema na maafisa elimu ili kuandaa mkakati wa nini kifanyike ili kuanza kutoa chakula ifikapo 1/5/2019 na atakae kaidi agizo hilo , watoe taarifa kwake ili kuona nini cha kufanya juu ya mtu huyo
“sasa ifike tarehe hiyo nikute mtendaji shule yake haijaanza kutoa chakula tutachukua hatua zingine kitu ambacho sitarajii kufika huko,kwahiyo mkalishughulikie suala hili kwa umakini”amesema Mallosa
Hata hivyo Ndg Mallosa ameongeza kuwa suala la chakula ni jukumu la mzazi hivyo mzazi au mlezi atakayegoma kuchangia chakula atawajibishwa kwa kufuata sheria inavyosema
Akizungumza katika kikao hicho Afisa Elimu Sekondari Bw. Alois Kaziyareli amesema kuwa mwaka jana mkuu wa wilaya ya Ulanga alizunguka wilaya nzima kuhamasisha suala la chakula mashuleni lakini baadhi ya shule hazikutoa chakula
Aidha ameongeza kuwa kwa suala la elimu bila malipo, chakula mashuleni na sare za shule ni jukumu la mzazi wa mtoto husika na si suala la serikali.
“Serikali inashughulika na mambo mengine yote lakini suala la chakula na sare za shule ni jukumu la mzazi au mlezi “Amesema Kaziyaeri .
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.